Mratibu
wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa Mama Ye unaoendeshwa na
asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la
Uingereza (DFID), Chiku Lweno akielezea jitihada zinazofanywa na mradi
wa Mama Ye katika kukabiliana na vifo vya Mama na mtoto ambapo aliwataka
waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelemisha jamii ili iweze
kuepukana na vifo vya mama na mtoto ambalo nalo ni janga la taifa.(Picha
zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Musoma
SERIKALI
imeshauriwa kuhakikisha sera na mipango mizuri iliyopo kwa afya ya mama
na mtoto mchanga inasimamiwa na kutekelezwa ili kuliondoa taifa katika
janga la kupoteza mama na watoto wakati wa uzazi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa Mawasiliano na uhamisishaji wa mradi wa
Mama ye unaoendeshwa na asasi ya Evidence for Action linalofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Chiku Lweno katika mafunzo
kwa waandishi wa habari mjini Musoma.
Alisema
bila kutekeleza mipango mizuri ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa
championi wa masuala ya wanawake na watoto kitaifa na mataifa, tatizo la
vifo kwa wanawake wenye pingamizi za uzazi na watoto wachanga.
Alisema
kutokana na haja ya kutoa msukumo katika masuala ya uzazi wameamua
kuwapatia elimu waandishi wa habari ili wawe chachu ya kutambua umuhimu
wa ukunga na uzazi salama.
“Tunafunza
waandishi wa habari ili waweze kusukuma mbele shahuri hili ili kila
mtu katika nafasi yake atetee nafasi yake” alisema Lweno.
Alisema
suala la mama na mtoto mchanga ni masuala mtambuka ambapo mambo mengi
lazima yaunganishwe yafikiriwe na kutambuliwa ili kudhibiti vifo vya
wanawake na watoto wachanga.
Alitaja
masuala hayo kama upangaji wa bajeti ya kueleweka kwa ajili ya kusaidia
kupatikana kwa wakunga wataalamu na vifaa vyao vya kazi na maeneo ya
kufanyia kazi. Aidha kuwapo kwa ukubali wa wakunga na elimu ya uzazi.
Alisema
ni vyema waandishi wa habari kama watia chachu kuelimishwa mambo mengi
yanayohusiana na uzazi salama ambapo ndani yake kuna masuala ya bajeti
na ufuaji wa wataalamu na ufuatuiliaji wa sera na sheria zilizopo katika
kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
Alisema anaamini waandishi wa habari wakielewa mambo hayo watasaidia kukomaa nalo na kuwezesha kila mtu kuwajibika.
Kaimu
Muuguzi Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Ama Kasangala akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja
yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA)
kuelekea kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga
duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mara.
Naye
Afisa Muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii,
Saturini Manangwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari alisisitiza
haja za waandishi kutambua dhana ya afya ya mama na mtoto kuwa ni kitu
mtambuka kutokana na suala la lenyewe kutegemeana.
Alisema
serikali inapohimizwa kuwekeza kwa mkunga kunatokana na ukweli kuwa
huduma ya mama na mtoto mchanga itakujwa bora kwa kuwa na mkunga bora
mwenye vifaa na anayefahamu wajibu wake kuanzia ujauzito wa mama hadi
kujifungua kwake.
Alisema
uwekezaji huo unagusia changamoto nyingi zilizopo sasa kama upungufu
wa wakunga, vituo vya kutolea huduma, dawa, miundombinu na masuala anuai
ambayo yameegemezwa na utambuzi wa bajeti na umuhimu wake kama
kipaumbele.
Alisema kwamba katika upangaji bajeti kila kitu kinategemea huwezi kusema unazidisha hiki na unakiacha hiki.
Alisema
mathalani katika hali bora ya ukunga na uwezo wa kumsaidia mhusika
,viwango vya dunia vilivyoweka na Shirika la Afya Duniani (WHO) kila
mkunga mmoja ahudumie angalau watu sita, lakini sehemu kubwa ya dunia
haifikii hivyo.
Aidha
alisema kwa Tanzania kiwango ni mkunga mmoja ahudumie watu 20-25 lakini
kwa sasa Tanzania mkunga mmoja anahudumia zaidi ya watu 50.
Kimsingi alisema Tanzania ina tatizo la wakunga na pamoja na serikali
kuanzisha vyuo vya kufunza wakunga na kukubali mashirika ya dini nayo
kufanya hivyo hali bado ni tete.
Hata hivyo alisema ni kupitia wakunga waliowataalamu upo uwezekano wa kuzuia vifo visivyo vya lazima.
Mratibu
wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akizungumzia nia ya
chama hicho ni kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa
anapata huduma za mkunga mtaalamu.
Muuguzi
huyo mwandamizi pia alisema katika juhudi za serikali kunaanzishwa
mafunzo ya mwaka mmoja ambapo yatatoa maofisa afya ambao kazi yao kubwa
itakuwa kujua idadi ya wanawake wajawazito na wagonjwa katika maeneo yao
na kutoa taarifa kwa zahanati iliyo karibu.
Alisema
ofisa huyo kazi yake haitakuwa hospitalini au kwenye zahanati bali
kwenye jamii akitambua idadi ya wagonjwa wake na kutoa taarifa sahihi ya
hali ya afya ya kitongoji chake kwenye zahanati.
Mmoja
wa washiriki Belina Nyakeke ambaye ni mwandishi wa habari wa magazeti
alisema kwamba amefurahishwa na mafunzo hayo ambayo yamempa nafasi ya
kutambua wajibu wake katika kusaidia kuondoa tatizo la vifo vya mama na
mtoto mchanga.
Alisema japokuwa mafunzo ni ya muda mfupi lakini yamemfumbua macho kutambua wajibu na haki kwa wananchi na serikali.
Naye
Ahmed Makongo akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemfanya atambue
wajibu wake kusaidia kusukuma mambo yaende sawa kwa upande wa waamuzi na
pia wananchi husika kwa kuzingatia mafunzo hayo yaliyoletwa kwao na
Mama Ye na UTTPC chini ya Ufadhili wa Shirika la Mpango wa watu Duniani
(UNFPA)
Afisa
muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Saturini
Manangwa akizungumzia changamoto za upungufu wa wakunga, vituo vya
kutolea huduma, dawa, miundombinu n.k wakati wa mafunzo kwa waandishi wa
habari wa mjini Musoma mkoani Mara.
Afisa
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) anayeshugulikia
mifumo ya Afya, Felista Bwana akitoa takwimu za nchi zinazoongoza kwa
vifo vya mama na mtoto kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mjini
Musoma.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen, mkoani Mara, Belina Nyakeke
(katikati) akishiriki kwenye mafunzo ya waandishi wa habari
yaliyofanyika mjini Musoma na kufadhiliwa na Shirika la UNFPA.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la Tanzania Daima mjini Musoma, Igenga Mtatiro
akiuliza swali kwa Afisa muuguzi mwandamizi kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Saturini Manangwa (hayupo pichani).
Pichani
juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Mara ambao pia
wanachama wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) walioshiriki
mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mradi wa Mama Ye kwa kushirikiana na
UTPC na kufadhiliwa na UNFPA.
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Rais
wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini
(TAMA), Martha Rimoy mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo.
Source http://sundayshomari.com
No comments:
Post a Comment