Sunday, March 15, 2015

Viongozi watakiwa kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi MUSOMA

Serikali wilaya ya Musoma mkoani Mara imewataka viongozi  katika  ngazi mbalimbali wilaya humo kuhakikisha inawalinda watu wenye ulemavu wa ngozi Alibinism na kutoa taarifa haraka katika vyombo vya dola kwa wale wote wenye njama za kufanya vitendo vya uhalifu dhidi yao.

Mkuu wa wilaya ya Musoma mkoani Mara Bw Zeloth Stiven ametoa kauli hiyo katika shule ya Msingi Mwisenge wakati Jumuiya ya wanachuo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare na Kanisa la Menonite Tanzania walipoungana na kwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo mafuta maalum ya kutumia kujipaka.

       Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi Mwisenge
                        Mkuu wa wilaya ya Musoma Bw Zelothe Steven

Alisema katika kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa viongozi na wananchi hawana budi kushirikiana ili kuhakikisha vitendo hivyo havitokei katika Manispaa ya Musoma.

"Viongozi lazima tupambane katika hili na ni lazima tushirikiane wote katika kuhakikisha hakuna mtu mwenye ulemavu wa ngozi hata mmoja anauawa katika wilaya yetu" alisema Mkuu huyo wa wilaya

Nao baadhi ya wanafunzi kutoka chuo cha Maendeleo  ya Jamii Buhare waliiomba serikali kuhakikisha inapambana na watu wanaohusika katika Mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika kuhakikisha watu hao wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
                           Mmiliki wa blog hii akishow love

Rais wa Jumuiya wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Bw Anania Piniel alisema kuwa kila mtu ana haki ya kuishi hivyo kuacha mauaji haya yaendeleo ni kuwanyima wengine haki ya kuishi hivyo serikali inapaswa kupambana na Mauaji haya.

 "Kuishi ni haki ya kila mtu na sasa kama watu hawa wataendelea kuuawa ni kuwanyima haki ya msingi ya kuishi,tunaiomba serikali ipambane na mauaji haya" alisema Bw Anania Piniel

No comments:

Post a Comment