Wednesday, August 20, 2014

POLISI MARA YAENDELEA KUJIFUA LIGI DARAJA LA KWANZA

KOCHA WA POLISI MARA AKITOA MAELEKEZO KWA WACHEZAJI

 TIMU ya soka ya maafande wa polisi Mara imeendelea kujifua kwenye viwanja vya posta mjini hapa katika kujiandaa na ligi daraja la kwanza huku wadau wa wakiombwa kuwa karibu na timu hiyo kuhakikisha inapanda ligi kuu msimu ujao.

Akizungumza na Blog hii kwenye mazoezi ya timu hiyo,msemaji wa timu ya polisi Mara Musa Keita amesema wachezaji wote waliofika kwenye mazoezi ya timu hiyo wanaendelea na mazoezi chini ya benchi la ufundi na wanashukuru mungu mazoezi yanakwenda vizuri na wamepata wachezaji wazuri.

No comments:

Post a Comment