Wednesday, June 11, 2014

WAMBURA KIDUME, APEWA RIDHAA NA TFF YA KUGOMBEA URAIS WA KLABU YA SIMBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Uchaguzi ya TFF, Julius Lugaziya (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa kamati hiyo kumrudisha mgombea wa Rais katika klabu ya Simba, Michael Wambura. Kulia Mkurugenzi Msaidizi Sheria na Wanachama TFF, Eliud Mvella.(Picha na Francis Dande)
Baadhi ya mashabiki wanaomuunga mkono mgombea wa nafasi ya Rais wa klabu ya Simba, Michael Wambura wakishangilia nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kamati ya Rufaa ya TFF, kumrejesha katika  kinyang’anyiro hicho.Picha na Francis Dande
--Shabiki wa Simba akifurahi kwa kuonyesha Katiba ya Simba.
 Mashabiki wa Simba wakionesha furaha yao klabuni Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.
Ilikuwa ni pata-shika nguo-kuchanika na pongezi motomoto kwa shujaa wao Wambura.
Sherehe za kumpongeza Wambura zikiendelea.
Chereko za kufa mtu zikiendelea mchana huu.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetupilia mbali pingamizi lililowekwa na wanachama wa Simba na kumruhusu mgombea wa nafasi ya urais katika klabu hiyo, Michael Wambura kuendelea na mchakato huo.
Mwenyikiti wa Kamati ya Rufaa wa TFF, Julius Lugazia alipotangaza rufaa hiyo alisema Wambura ni mwanachama halali wa Klabu ya Simba kisheria hivyo anayo haki ya kugombea nafasi hiyo kama wagombea wengine kwani amekuwa akishirikishwa katika kamati mbalimbali huku mchango wake wa kimawazo ukitumika ndani ya klabu hiyo
Mashabiki wa Klabu ya Simba ambao ni wafuasi wa Wambura, walipokea taarifa hiyo ya TFF kwa mikono miwili na kushangilia kwa staili ya kipekee kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kwa kufurahishwa na maamuzi hayo.
 (Picha na Stori Deogratius Mongela GPL)

No comments:

Post a Comment