Monday, May 19, 2014

Taifa Stars yaanza Afcon 2015 vyema

                Bocco adebayooooooooooooooooo
                               Kikosi cha Taifa Starz
            Dida shujaa wa Mchezo

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta (juu) akikwepa kwanja wakati akijaribu kumtoka beki wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 zinazotarajia kufanyika nchini Morocco, wakati wa mtanange huo uliopigwa May 18,2014 kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Taifa Stars, ilishinda bao 1-0.


......Bao la Stars limefungwa na John Bocco 'JB' dakika ya 16 kipindi cha kwanza.......

Timu ya Tanzania-Taifa Stars, ikicheza nyumbani kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, May 18, 2014, imeifunga Zimbabwe bao 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya AFCON 2015 kuwania kucheza Fainali huko nchini Morocco Mwaka 2015.
Katika Mechi hiyo, bao pekee na la ushindi kwa Taifa Stars lilifungwa na Straika wa Azam FC, John Bocco, katika Dakika ya 15 baada kuunganisha Krosi ya Thomas Ulimwengu anaecheza TP Mazembe ya Congo DR.
Kocha wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij alisema baada ya mchezo huo kwamba vijana wake wamecheza vizuri, lakini wangeweza kupata mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Kwa upande wake, kocha mzalendo wa Zimbabwe, Ian Gorowa alisema vijana wake walicheza vizuri, lakini walikosa bahati ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri.
Timu hizi zitarudiana huko Harare Wikiendi ya kuanzia May 30,2014  na Mshindi atacheza na Mshindi kati ya Mozambique na South Sudan kwenye Raundi inayofuata ambayo ndio itatoa Timu moja kuingia KUNDI F kujumuika na Zambia, Niger na Cape Verde.
Katika mechi nyingine jana, mabao mawili ya Frank ‘Gabadinho’ Mhango yaliipa Malawi ‘The Flames’ ushindi wa 2-0 dhidi ya Chad Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, nao Sao Tome Principe walifungwa 2-0 nyumbani na Benin, Namibia iliilaza 1-0 Kongo na Mauritania iliibwaga 1-0 Equatorial Guinea.
AFCON 2015-MOROCCO: DROO YAFANYIKA.
DROO ya Mashindano ya Mataifa ya Africa, rasmi kama Orange Africa Cup of Nations Morocco 2015, ambayo Fainali zake zitachezwa huko Morocco kati ya Tarehe 17 Januari hadi 8 Februari 2015, imefanyika hii Leo huko Cairo, Egypt.
Nchi 51 zitashiriki Mashindano haya ambapo Mauritania na South Sudan zilishinda toka Raundi ya Kwanza na kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano ambayo Tanzania itacheza na Zimbabwe.
Washindi 14 wa Raundi ya Pili ya Mtoano wataingia Raundi ya Tatu ya Mtoano ili kupata Timu 7 zitakazosonga kwenye Makundi ambayo hii Leo pia yamepangwa.
Ikiwa Tanzania itaitoa Zimbabwe basi kwenye Raundi ya Tatu ya Mtoano itacheza na Mshindi kati ya Mozambique na South Sudan na Tanzania ikipita hapo itaingia KUNDI F ambako ziko Zambia, Cape Verde na Niger.
Yapo Makundi 7 ambapo Mshindi wa Kila Kundi na Mshindi wa Pili wa Kila Kundi pamoja na Timu moja iliyofuzu Nafasi ya 3 Bora katika Makundi ndizo zitaingia Fainali kuungana na Morocco na kufanya idadi ya Timu 16 kwenye Fainali.
RATIBA/MAKUNDI.
Nchi ambazo zimeingia Makundi moja kwa moja:-
Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Zambia, Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria, Angola, Cape Verde, Togo, Egypt, South Africa, Cameroon, DR Congo, Ethiopia, Gabon, Niger, Guinea, Senegal and Sudan.
RAUNDI YA PILI YA MTOANO.
Mechi Na 1: Liberia vs Lesotho
Mechi Na 2: Kenya vs Comoros
Mechi Na 3: Madagascar vs Uganda
Mechi Na 4: Mauritania vs Equatorial Guinea
Mechi Na 5: Namibia vs Congo
Mechi Na 6: Libya vs Rwanda
Mechi Na 7: Burundi vs Botswana
Mechi Na 8: Central African Republic vs Guinea Bissau
Mechi Na 9: Swaziland vs Sierra Leone
Mechi Na 10: Gambia vs Seychelles 
Mechi Na 11: Sao Tome e Principe vs Benin
Mechi Na 12: Malawi vs Chad
Mechi Na 13: Tanzania vs Zimbabwe
Mechi Na 14: Mozambique vs South Sudan
**Mechi za Kwanza 16,17,18 Mei 2014
**Mechi za Marudiano 30,31 Mei au 1 Jun1 2014
RAUNDI YA TATU YA MTOANO.
**WASHINDI 14 wa Raundi ya Pili ya Mtoano watacheza Raundi hii

No comments:

Post a Comment