Sunday, May 11, 2014

Man city watwaa ubingwa wa Uingereza

Manchester City wamechukua Ubingwa wa Ligi kuu Soka Uingereza Msimu wa 2013/2014 -leo May 11, 2014, mara mbili ndani ya misimu mitatu, mara ya mwisho walikuwa mabingwa msimu we 2011-12…Msimu uliofuata wa 2012-13, majirani zao Manchester United wakalibeba lakini msimu huu wakawa nyanya na Man City wameendelea kulibakiza jijini Manchester.

Man City imebeba kombe hilo baada ya kuitwanga West Ham kwa mabao 2-0 huku Liverpool nao wakishinda kwa 2-1 dhidi ya Newcastle huku Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasri na nahodha Vincent Kompany wakati Liverpool walianza kwa Skirtel kujifunga kabla ya Daniel Agger na Daniel Sturridge kusawazisha na kuongeza….Liverpool wameshindwa kuifikia Man City kwa pointi 2, walichokuwa wanaomba leo ni  Man City kupoteza na wao washinde, ili watwae Ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 24.

Chelsea imemaliza katika nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Cardiff City kwa mabao yaakifungwa na  Schurrle dakika ya 72 na Torres dakika ya 75, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Bellamy dakika ya 15.

Arsenal imemaiza katika nafasi ya nne kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Norwich City, mabao ya Ramsey dakika ya 53 na Jenkinson dakika ya 62. 
Everton iliyoifunga 2-0 Hull City imemaliza katika nafasi ya tano, wakati Tottenham Hotspur imemaliza ya sita baada ya kuifunga 3-0 Aston Villa na Manchester United iliyotoa sare ya 1-1 na Southampton  imemaliza ya saba.

Cardiff 1 - 2 Chelsea 
Fulham 2 - 2 Crystal Palace
Hull 0 - 2 Everton 
Liverpool 2 - 1 Newcastle
Man City 2 - 0 West Ham
Norwich 0 - 2 Arsenal
Southampton 1 - 1 Man Utd
Sunderland 1 - 3 Swansea
Tottenham 3 - 0 Aston Villa
West Brom 1 - 2 Stoke

No comments:

Post a Comment