Monday, May 19, 2014

Kinana akamilisha ziara yake Mkoani Tabora

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo jioni kwenye Uwanja wa Stendi ya zamani mjini Tabora. Kinana amemaliza ziara yake ya siku 11 leo,Mei 18, 2014.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa Tabora mjini.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, bunge wa Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira akihutubia kwenye mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza serikali ilivyotekeleza ilani yake ya uchaguzi hadi sasa.

 Mbunge wa Sikonge, Said Mkumba kwenye mkutanbo huo ambapo pamoja na mambo mengine, ameomba sheria zianze kufuatwa kwa viongozi wa siasa kutojishirikisha na vyama vya ushirika ili kutochanganya amaslahi.

 Mbunge wa Viti Maalum, Ummy Mwalimu akihutubia kwenye mkutano huo na kueleza mambo mbalimbali muhimu kuhusu mchakati wa katiba mpya.
 Mbunge wa Jimbo Mtera, Joseph Lusinde akihutubia kwenye mkutano
 Matukio yakienda live kwa kupitia simu. Kulia ni Mbunge wa Nzenga, Hamis Kigwangala.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, akieleza  utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyofanywa na serikali katika huduma ya maji nchini na husuasan mkoa wa Tabora
 Mmoja wa Wazee waasisi wa CCM Tabora akipiga picha ya ukumbusho kwenye mkutano huo
 Mbunge wa Urambo, Samuel Sitta akiwasalimia wananchi kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa Stendi ya zamani ya mabasi mjini Tabora
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi na msafara wake kwenda kwenye mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, wakila chakula kwa Mama Lishe wa kwenye stendi mpya ya mabasi mjini Tabora kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila chakula cha Mama lishe wa Tabora mjini stendi mpya ya mabasi kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara, Kushoto ni Mbunge wa Tabora Aden Rage na Viti Maalum Munde Tambwe.

No comments:

Post a Comment