Thursday, May 22, 2014

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA ARUSHA

Meneja Biashara wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Brighton Majwala (kushoto) akizungumza jambo na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Alumeru, Nyirembe Munasa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi  wa duka la huduma kwa wateja jijini Arusha.Katikati ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba(wa pili kushoto) na Maneja wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA, Inginia Annette Matindi.
Mkuu wa Wilaya ya Alumeru, Nyrembe Munasa akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel jijini Arusha .Kutoka kushoto ni Meneja Biashara wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Brighton Majwala, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba na Maneja wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA, Inginia Annette Matindi.
Mkuu wa Wilaya ya Alumeru, Nyrembe Munasa akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa duka la huduma kwa wateja la airtel jijini Arusha .Kushoto ni Meneja Biashara wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Brighton Majwala.Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini Arusha leo.
Meneja Biashara wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Brighton Majwala ( wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Alumeru, Nyirembe Munasa(kushoto), Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba(kulia) na Maneja wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA, Inginia Annette Matindi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi  wa duka la huduma kwa wateja jijini Arusha leo.
Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,tawi la jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara bada ya uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja leo.
Airtel yazindua duka la Arusha
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za kibunifu  nchini leo imezundua duka lake lakisasa  lililopo jijini Arusha
Ufunguzi wa duka hilo ulizindulia na Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Akiongea wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba alisema” Leo tunazindua duka la pili la kisasa baada ya kuzindua duka letu la Xpress lililopo Mlimani City mwishoni mwezi ulipita. Hii ni kwasababu tunaamini katika kutoa na kuwapatia wateja wetu huduma bora na za kifunibu na  uzinduzi wa leo ni mwendelezo wadhamira yetu ya  kuleta huduma za kisasa zinazowahakikishia wateja wetu usalama na huduma bora wakati wote”.
Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora kote nchini na kwa wakazi wa Arusha sasa wataweza kufurahia huduma zetu katika mazingira bora na yaliyoboreshwa zaidi.Duka hili limetengenezwa kwa kisasa likiwa na uwezo wa kuwawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi  bila usumbufu huku wafanyakazi wetu wakipata mazingira bora ya kufanyia kazi na kuleta ufanisi mkubwa.”
 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bwana Nyirembe Munasa alisema” Nawashukuru sana Airtel kwa kuongeza wigo kupitiia huduma kwa wateja na kuleta mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu utaleta hari kwa wafanyakazi na pia na kuongeza nafasi za ajira lakini sambamba na hayo pia utawawezesha wakazi wa Arusha kupata huduma bora wakati wote na kwa hilo Tunawashukuru sana Airtel”
Natoa wito kwa wakazi wa Arusha na wateja wa Airtel kutembelea duka hili la Airtel Xpress na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa ikiwemo huduma ya Airtel Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha ikiwemo kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi zaidi aliongeza Munasa
Airtel itaendelea kuzindua maduka yake nchi nzima ili kufanya sehemu za kutoa huduma zao kuweza kufikiwa kirahisi
 
Source Gsengo

No comments:

Post a Comment