Friday, March 21, 2014

Wahariri wa makala wataka ushirikiano habari za uchunguzi


Wahariri wa makala kutoka katika Gazeti la Mwananchi Nevil Meena pamoja na Peter Olwa kutoka katika gazeti la Uhuru, wamewaaomba wahariri wa  vyombo vingine vya habari kutoa ushirikiano katika kazi za uchunguzi wanazofanya waandishi wa habari kutoka vijijini.
 
 Nevil Meena ni Mhariri wa Makala kutoka gazeti la Mwananchi (1)
Maelezo hayo wameyatoa katika mafunzo maalum yaliyofanyika Morogoro.
 
“Tunawaomba wahariri wenzetu kuwapa ushirikiano wanahabari pindi wanaporudi kutoka katika kazi za uchunguzi, kwa kutumia makala zao ili kuweza kuleta chachu ya uwajibikaji kwa viongozi sehemu mbalimbali za vijijini hapa nchini, ni makosa kwa mhariri kupokea rushwa kutoka kwa mwandishi wa habari, pia ni kosa na mwandishi kutoa pesa ya hongo kwa mhariri ili aitumie stori yake,” alisema Meena.

Aidha Meneja mafunzo wa Tanzania Media Fund (TMF), Radhia Mwawanga, amewashauri waandishi wa habari kuandika habari zilizo makini, kwa sababu habari ikiwa imechunguzwa kwa undani mhariri lazima ataitumia iwe kwenye gazeti, redio au televisheni.
 
source>taarifa newz

No comments:

Post a Comment