Tuesday, January 7, 2014

Zana haramu za uvuvi zateketezwa mkoani Mara

MUSOMA
 
Serikali Mkoani Mara imezitaka halmashauri za wilaya mkoani humo kukusanya Mapato na kisha sehemu ya Mapato hayo kutumika katika kupambana na Vitendo vya Uvuvi haramu vinavyofanyika ndani ya Ziwa Victoria.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa alisema hayo wakati wa kuteketeza zana haramu zaidi elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia tatu kufuatia Operesheni za doria zilizoendeshwa na kikosi cha doria,Maafisa Uvuvi,Polisi na BMU mkoani hapa.
Bw Tupa ambaye alichoma zana hizo haramu amesema Uvuvi huo utakwisha kama kutakuwa na Ushirikiano kuanzia kwa Wanasiasa na kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara ndani ya ziwa Victoria na Maduka yanayouza zana hizo.

Kwa upande wake afisa Mfawidhi Msimamizi na Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi mkoani Mara Bw Braison Gasper Meela alisema zana hizo haramu zinateketezwa kwa Mujibu wa Kanuni ya Uvuvi ya Mwaka 2009 ambayo inapiga Marufuku Kutengeneza,kuhodhi,kuuza au kumiliki na kutumia Zana hizo katika shughuli za Uvuvi ndani ya Ziwa Victoria.
 
Zana hizo haramu ambazo zimeteketezwa ni  pamoja na Kokoro 652,Nyavu utali 4084,Nyavu za tupatupa 40,Nyavu za Makila 8774,Kamba za Kokoro 53020 na vyavu za Dagaa 28.
 
             Matukio katika Picha
                            Bw John Gabriel Tuppa

No comments:

Post a Comment