Friday, January 10, 2014

Mama Maria azindua shule ya Sekondari ya J.K Nyerere iliyojengwa na Mgodi wa African Barrick North Mara

TARIME
Watanzania wametakiwa kuheshimiana na kuvumilia ili Mawazo yanayotolewa katika Jamii yatumike kuleta Maendeleo kiroho na Kimwili katika sehemu mbalimbali hapa nchini na Taifa kwa ujumla


Hayo yameelezwa na Mke wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mama Maria Nyerere wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wilaya ya Tarime Mkoani Mara katika uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Julius Kambarage Nyerere iliyojengwa na Mgodi wa African Barrick North Mara.
Mama Maria alisema kuwa kila jambo linahitaji uvumilivu na kuheshimu mawazo ya kila mmoja ili kujenga umoja na Mshikamano katika Jamii.
                            Mjane wa Baba wa Taifa mama Maria nyerere kulia
              
Awali akimkaribisha Mama Maria Nyerere,Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa ameshauri kujengwa Makumbusho ndogo katika taasisi mbalimbali ambazo zinapewa jina Mwalimu Nyerere huku Meneja wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo umegharimuaidi ya  shilingi Bilioni mbili huku akisema kuwa Mgodi huo utaendelea kuimarisha na kutekeleza Miradi mbalimbali katika maeneo hayo ya Mgodi.

Katika hatua nyingne Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga wameelezea kufurahiswa na utekelezaji wa Miradi hiyo inayofanywa na Mgodi wa African Barrick North Mara na kusema hayo hayo ndiyo Matunda ya Ushirikiano huku wakisifu jitihada za Serikali kuleta wawekezaji ambao wamekuwa na tija kwa Jamii

                                              HABARI KATIKA PICHA

                   Mkuu wa wilaya ya Butiama akinena jambo na Meneja wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman
                                      Bw Fanuel Nicholaus akisoma risala
                                Meneja wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman
            Mama Maria Nyerere akifurahia jambo baada ya uzinduzi wa JK nyerere Sekondari

No comments:

Post a Comment