ZANZIBAR
 JUMAMOSI JANUARY 18, 2014. Jeshi la Polisi Zanzibar linamshikilia 
Askari mmoja wa Chuo cha Mafunzo sawa na Magereza kwa Tanzania Bara 
Sajin Meja (S/Sgt) Hassan Iddi Hassan (45), kwa tuhuma za wizi wa 
shilingi 1,635,000 alizoziiba kutaka katika duka moja lililopo eneo la 
Makadara mjini Zanzibar.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, 
amesema
 tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.00 jioni wakati  Askari huyo
 akiwa amevaa kiraia, alipofika katika dukani kama mteja wa kawaida 
huku  muuzaji wa duka hilo akiwahudumia wateja wingine na ndipo 
alipoingia ndani na kufungua droo ya pesa na kuiba kiasi cha shilingi 
1,635,000 na kuanza kutimua mbio.
Inspekta
 Mhina, amesema hata hivyo askari huyo alitiwa nguvuni na Polisi baada 
ya kufukuzwa na wananchi na kukutwa akiwa na fedha  zote alizoiba na kuokiolewa.
Naye
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Mkadam Khamisi 
Mkadamu, amesema kuwa fedha zote zilizoibwa na kupatikana mikononi mwa 
Askari huyo zimehifadhiwa Polisi ikiwa ni kielelezo mahakamani.
Hilo
 ni tukio la tatu kutokea mjini Zanzibar katika kipindi cha mwaka huu 
ambapo tukio la kwanza ni lile la jaribio la wizi katika maghala ya 
Bakheresa eneo la Fuoni nje kigodo ya mji wa Zanzibar ambapo watuhumiwa 
watatu walikamatwa wakiwa na silaha aina ya gobore linalotumia risasi za
 short gun.
Na
 tukio linguine ni la kukamtwa kwa majambazi wanne akiwemo Afisa wa 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini wakiwa na silaha tatu 
zikiwemo bastola mbili na SMG moja
 baada ya kumvamia mfanyabiashara mmoja na kumpora milioni 11.5 eneo la 
Rahaleo mjini Zanzibar.
Matukio
 hayo yote yakiwa na jumla ya watuhumiwa wanane na silaha nne yaliweza 
kukabiliwa kwa haraka na Polisi kufuatia msaada wa wananchi wa kutoa 
taarifa za haraka polisi na wenyewe kujitolea kusaidiana na Polisi 
kuwakabili watuhumiwa na kufanikisha ukamataji salama.

No comments:
Post a Comment