Tuesday, January 7, 2014

Zaidi ya tani Elfu nane za Chakula zinahitajika Butiama mkoani Mara


BUTIAMA

Zaidi ya tani elfu nane za Chakula zinahitajika katika wilaya ya  Butiama mkoani Mara ili kukabiliana na tatizo la njaa kali ambalo limeikumba wilaya hiyo na Wananchi kushindwa kufanya shughuli za Maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Butiama mkoani Mara Bw Josephat Maganga ameelezea upungufu wa Chakula ulipo katika halimashauri hiyo katika kikao cha bajeti cha barza la Madiwani na kusema kuwa tayari halmashauri hiyo hiyo imepeleka ombi maalum katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Amesema baada ya Tathimini iliyofanywa na halmashauri hiyo imebaini kuwepo kwa tatizo kuwa la njaa ambapo tani 8554.5 za Chakula  zinahitajika katika kukabiliana na tatizo hilo la njaa katika halmashauri hiyo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Butiama BW Magina Magesa amesema kutokea kwa tatizo la njaa katika halmashauri hiyo lisionyeshe kuwa wananchi wa Maeneo hayo ni wavivu katika suala la Kilimo bali ni kutokana na ugonjwa wa Mihogo ulioikumba halmashauri hiyo

katika Mwaka ujao wa fedha halmashauri hiyo imeeleza kupeleka Tamisemi na hazina Maombi maalum ya Miradi Mikubwa ambayo ni ujenzi wa jengo la Utawala katika hospital ya Butiama,Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, ununuzi wa Magari Manne,Ujenzi wa barabara ya kilomita 14na ujenzi wa Jengo la Utawala katika Hamashauri hiyo  ambapo miradi hiyo itagharimu kiasi cha shilingi billion 6.7

No comments:

Post a Comment