Mabalozi
wa nyumba kumi katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara wameiomba serikali
kuwakumbuka na kuweka utaratibu maalum wa kuwatambua kutokana na kuwa karibu na
Jamii na hivyo kusaidia katika suala la ulinzi na Usalama katika maeneo yao.
Hayo yameelezwa
katika kikao ya siku moja ya mabalozi 600 kutoka Mitaa 57 ya halmashauri ya
Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambapo kikao hicho kilikuwa na lengo la
kutathimini Changamoto zinazowakabili Mabalozi likiwemo suala la ulinzi na
Usalama katika maeneo yao.
Wakiongea
katika Warsha hiyo baadhi ya Mabalozi walipata nafasi ya kuongea wamesema
kumekuwepo na lawama kutoka nyumba wanazoziongoza kutokana na ahadi hewa zinazotolewa na baadhi ya viongozi,wengine
wakisema kwasasa wamebaki kuwa mabalozi wa kutangaza msiba huku wengine
wakiongeza kuwa mabalozi wamebaki kama punda.
"Sisi ndiyo tuko karibu sana na wananchi kama ni wau wabaya tunawajua sisi lakini hatupewi thamani mpaka wakati wa uchaguzi unapofika" alisema Bi Sofia
Kwa
Upande wake Mjumbe wa UWT Taifa kutoka mkoani Mara Bi Agnes Methew amewataka
Mabalozi kuvunja Makundi ambayo yamekuwa yakikigharimu chama cha Mapinduzi nyakati
za Uchaguzi na kuiomba Serikali kuwataza mabalozi na kuwatambua kama kiungo
muhimu.
"Kabla ya wote ebu tuache kwanza Makundi ambayo si mazuri ndani ya Chama lakini pia tunamuomba Rais Kikwete awatazame maana anatambua umuhimu wenu" alisema Bi Agnes
PICHA MBALIMBALI ZA MABALOZI KATIKA KIKAO HICHO
No comments:
Post a Comment