RORYA
Chama cha
Mapinduzi (CCM) wilaya ya Rorya Mkoani Mara kimewataka wanachama na wapenzi wa
Chama hicho kuungana katika Mwaka 2014 kuhakikisha Chama hicho kinafanya vizuri
katika Chaguzi zinazokuja huku kikiwatahadharisha wale wote wenye kuleta
Makundi ndani ya Chama.
Kauli
hiyo ilisemwa na Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi CCM wilaya Rorya Bw Samweli
Kiboye katika kikao cha halmashauri kuu cha wilaya hiyo kilichofanyika Mwishoni
mwa Mwaka 2013 katika wilaya hiyo.
Amesema
kama Chama hicho kitawaogopa wale wote wanaleta Makambi ndani ya Chama kazi itakuwa
ngumu kwa Chama hicho katika chaguzi zinazokuja
"Kumekuwa na watu wasiotakia CCM mema wamekuwa wakileta makundi makundi tu ndani ya Chama,sasa hatutakubali wale wote wanaoleta Makundi ndani ya Chama"alisema Mwenyekiti huyo
Baadhi ya wanaCCM wakiwa katika halmashauri kuu
Kwa
Upande wake Katibu wa CCM katika wilaya hiyo Dr Fikirini Masokola alisema kiongozi yeyote wa Serikali ambaye atashindwa kutimiza Matarajio ya Chama hicho
ndani ya wilaya ya Rorya hawatahitaji kuwa nae katika wilaya hiyo.
"Hatutakubali kuwa na kiongozi yoyote ambaye hatatimiza Matakwa ya Serikali kwa wanaRorya" alisema Dr Fikirini Masokola
Katika
Kikao hicho Chama cha Mapinduzi CCM kilitoa hati ya Pongezi kwa baadhi ya watu ambao wametoa ushirikiano
ndani ya Chama hicho kwa Mwaka 2013 huku kikiwaomba kuendeleza ushirikiano wao
katika Chama hicho kwa Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment