Sunday, December 8, 2013

Akatwa sikio na Sime kwa kukataa kufanya Ngono na Shemeji yake

 Muuguzi wodi ya wanawake hospitali Teule ya Nyerere wilayani Serengeti akimtibu jeraha  Ghati Mikere(20)mkazi wa Kijiji cha Bisarara wilaya humo  anayedaiwa kukatwa shingo na sikio  na shemeji yake baada ya kukataa kufanya naye ngono. 
 Ghati Mikere akiuguza majeraha
 
Mratibu wa dawati la polisi la Jinsia WP Sajenti Sijali Nyambuche akichukua maelezo ya Ghati walipotembelea majeruhi mbalimbali hospitalini hapo

Serengeti:
 
WAKATI wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali wakiwa katika kampeini za kupinga vitendo vya  ukatili wa kijinsia,Ghati Mikere(20)mkazi wa Kijiji cha Bisarara wilaya ya Serengeti amenusurika kufa kufuatia kukatwa shingo na sikio baada ya  kukataa kufanya ngono na shemeji yake .
 
Tukio hilo lililompelekea kulazwa wodi ya wanawake hospitali ya wilaya ya Nyerere limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali,linadaiwa kutokea novemba 30 mwaka huu majira ya saa 5:asubuhi nyumbani kwa majeruhi huyo.
 
Akiongea kwa kugugumia  kutokana na maumivu akiwa wodini alisema shemeji yake Chacha Kitari alimkata baada ya kukataa kushiriki tendo la ngono kwa madai ya kuondoa mkosi wa mme wake kufungwa jela ,alipokataa ikapelekea kukatwa sikio la kushoto na  shingo.
 
“Kabla ya kunishambulia kwa fimbo na kunikata kwa sime…alinitaka nifanye naye ngono kwa madai kuwa ni maamzi ya ukoo na itasaidia kuondoa mkosi kwenye ukoo…kisha amiliki mji na ndiye awe mme wangu ..yaani wameishajipanga kama mme wangu anafia huko”alisema kwa masikitiko.
 
Hata hivyo Ghati hakuwa tayari kusema mme wake kafungwa miaka mingapi na kwa kosa lipi,na ameanza kutumikia kifungo lini.
Alisema licha ya kupiga kelele kuomba msaada ,ndugu walimpuuza na ndipo akapata msaada kwa majilani wa kufika hospitali kwa kupitia polisi.
 
Mkuu wa kituo cha Polisi Mugumu ASP Joseph Maganga ambaye aliongoza dawati la jinsia akiwa hospitalini hapo alisema ,wanaendelea kumsaka mtuhumiwa kwa kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yameshamiri na kuomba jamii kutoyafumbia macho kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwenye familia na taifa.
 
Katika tukio jingine  mwanamke mmoja Mgosi Chacha (20) mkazi wa mtaa wa bomani mjini Mugumu naye amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya na mme wake wa kufikia kwa madai ya kukataa kurudisha  mahari iliyotolewa na mwanamke aliyemuoa(Nyumba Nthobu).
 
Akiwa wodi la wanawake mbele ya dawati la jinsia la polisi alisema desemba  2.majira ya saa tatu usiku mwaka huu akiwa nyumbani kwake mtaa wa  bomani mwanamme huyo  Chacha Charles mkazi wa kijiji cha Bonchugu alimfanyia unyama huo baada ya kudai hatarudisha mahari ya mwanamke huyo kwa kuwa aliolewa kwa mila na desturi za Kikurya.
 
“Nimeolewa kwa ng’ombe 12 kutoka kwa bibi Bhoke Charles …ndoa ya Nyumba Nthobu…huyo mwanamme yeye ameteuliwa na ukoo wa bibi ambaye alinitolea mahari…ambaye hakuzaa na ameishakuwa marehemu …amenizalisha watoto wanne ambao ni mali ya alinitolea mahar”alisema.
 
Alisema siku ya  tukio Charles akiwa nyumbani mtuhumiwa huyo alifika na kusema anataka  ng’ombe hao kwa kuwa amemweleza muda mrefu bila utekelezaji,na kumpa nafasi ya kujibu na alianza kumshambuli na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili,kana kwamba haitoshi alimchukuakua usiku huo akiwa ajitambui na kwenda kumtupa kwenye shimo refu umbali wa kilomita 2 kutoka nyumbani kwake ambapo aliokotwa asubuhi na wapita njia ambao walitoa  taarifa polisi na yeye alipata fahamu na kujikuta  amelazwa hospitali.
 
“Kwa sasa hali za wanawake hao zinaendelea vizuri na wanapata huduma ya matibabu ,  tofauti na mwanzo walipofikishwa Hospitali walikuwa katika hali mbaya”,alisema  Musa Wilison Muuguzi mwandamizi msaidizi .

No comments:

Post a Comment