Tuesday, November 19, 2013

WANAHABRI WAKUMBUSHWA KUANDIKA HABARI ZENYE UKWELI

 Mwezeshaji wa Mafunzo ya uboreshaji wa uandishi wa habari katika Mitandao (Blog) kutoka Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) Beda Msimbe Kulia akitoa ufafanuzi huku akisikilizwa na Mwezeshaji mwenzake Bw Saimon Mkina katikati

Waandishi wa habari nchini wametakuwa kuwa wakweli katika kuandika habari mbalimbali wanazoziandika zikiwemo za Uchunguzi katika kusaidia Jamii inayowazunguka.

Hayo yameelezwa na Mwezeshaji wa Warsha ya siku tano ya Uboreshaji wa Uandishi wa habari katika Mitandao ya Kijamii  Bw Simon Mkina Mkoani Dodoma.

Alisema mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Mfuko   wa  vyombo  vya habari  Tanzania (TMF) yameelezwa yatakuwa Msaada Mkubwa kwa Wanahabari wanaoandika katika Mitandao ya kijamii kwani asilimia kubwa ya wanahabri kwasasa wamekuwa wakitoa taarifa za Matukio badala ya kufanya uchunguzi.

Bw Mkina alisema kuwa uandishi wa habari za Uchunguzi  utakuwa na Msaada Mkubwa katika Jamii kwani kinachotakiwa na mhusika kuandika vitu vya kweli na kufuata maadili ya uandishi wa habari.

Katika  hatua  nyingi  Mkina alitaka  wanahabari hao  na  wengine ambao  hawajapatiwa mafunzo ya  uboreshaji  wa habari za mkitandaoni ni  vema  sasa  kurejea katika maadili .

Kwa upande wale  mkufunzi  wa mafunzo hayo Bw Beda Msimbe  alisema  kuwa lengo la kuanzisha mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza  kufanyika ni  kutoka kuongeza ubora  wa uandishi  unaozingatia maadili katika mitandao  hiyo .

Msimbe  alisema  kuwa usalama  wa wanahabari  utaendelea  kuwa hatarini iwapo  wanahabari hawataheshimu maadili  na kuendelea  kutumika kwa  kuchafua  ama  kufanya uandishi  usio  zingatia maadili.

 Kwa  upande  wake afisa miradi wa TMF  Japheth Sanga  aliwataka  wanahabari hao  mbali ya kuandika habari za uchunguzi kuhakikisha  wanaheshimu sheria za nchi .

No comments:

Post a Comment