Friday, November 29, 2013

UVCCM Butiama waanzisha Siasa na Uchumi

KUTOKA BUTIAMA - Mara
Vijana nchini wametakiwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji Mali katika kujipatia kipato ikiwa ni njia ya  kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kutimiza Malengo yao.

Kauli hiyo ilitolewa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilaya ya Butama mkoani Mara katika baraza la Vijana la wilaya hiyo lilofanyika Butiama mkoani  hapa.

  Bwana Gerald Joseph. Mwenyekiti wa VCCM. Butiama Bunda Mara

       Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Butama mkoani Mara Bw Gerald Joseph alisema  Vijana wilayani humo wamefia hatua ya kufanya Siasa na Uchumi kama njia ya kujikwamua katika lindi la Umaskini na kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa.

 " Tumeamua kufanya Uchumi na siasa na hii itatusaidia kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa ambao Mara nyingi huwatumia vijana na Mwisho wa siku  kijana hubaki bila msaada" alisema Mwenyekiti huyo

Katika kufanya siasa na Uchumi Mwenyekiti huyo alisema kuwa vitega uchumi mbalimbali vitaanzishwa katika mikakati ya kujikomboa kiuchumi aambapo sehemu kubwa watajikita  katika kilimo na ujenzi wa hostel za kupangisa.

Katika hatua nyingne baadhi ya Vijana ambao ni wajumbe katika Baraza hilo waliwaasa vijana wenzao kutotoa mwanya kwa wanasaisa kuwatumi bali wajipange katika kufanya siasa na Uchumi kama njia ya kutokuwa ombaomba.

Walisema kutofanya hivyo wataendelea kuwalalamikia Viongozi kuwa wanawathamini hasa nyakati za uchaguzi jambo ambalo walisema wanalipinga.

     " Lazima tujitegemee sisi wenyewe hasa kwa kufanya siasa na Uchumi kuliko kuwategemea wanasiasa ambao dakika ya mwisho baada ya kufanikiwa hatuwaoni" alisema Julius mmoja wa wajumbe wa baraza hilo

No comments:

Post a Comment