Wednesday, November 6, 2013

WATENDAJI WABOVU WA SERIKALI WACHUKULIWE HATUA -NAPE

Wanaokiuka Maagizo ya Serikali na haki za Binadamu kukiona

TARIME

Chama cha Mapinduzi CCM kimetaka kuchukuliwa hatua kwa baadhi ya Watendaji wa Serikali ambao wameshindwa  kusimamia sheria na taratibu zilizowekwa katika kusimamia na kusababisha kuwepo kwa Migogoro katika Jamii.


Katibu wa itikadi na uenezi Taifa wa CCM  Bw Nape Nauye alito kauli hiyo katika Mji wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara,wakati akiongea na wananchi wa mji huo kwa nyakati tofauti.

Alisema kumekuwepo na malalamiko katika eneo hilo likiwemo la Polisi dhidi ya raia,ulipaji wa fidia,Maji ya Sumu yanayodaiwa kutoka Mgodi wa North Mara,Mfuko wa elimu katika eneo hilo na wachimbaji wadogo wa dhahabu.

"Haiwezekani upewe nafasi ya kuwasaidia wananchi lakini unashindwa kufanya hivyo na badala yake kufanya unavyotaka,Serikali lazima iwachukulie hatua Wafanyakazi wa aina hii" alisema Nape

Awali wakiongea katika Mkutano wa ndani baadhi ya wananchi wametoa Malalamiko yako Kwa katibu huyo ambapo walisema kuwa yamekuwa kikwazo katika kukamilisha yale ambayo yamekusudiwa na serikali .


''Ndugu katibu hawa watendaji ndiyo tatizo kwa Serikali kukamilisha yale yaliyokusudiwa mimi nadhani wafukuzwe tu kazi" alisema mzee Marwa Weitara

Kuhusu tatizo la Maji Machafu yanayotoka katika Mgodi wa North Mara,Nape alisema kuwa hilo ni tatizo kubwa ambalo serikali inapaswa kuchukua hatua 

"Hili suala la Maji nimeliona mwenyewe na kilichonishangaza ni kwamba yale Maji ni meupe lakini pale yanapopita ni Peusi sana hii ni hatari,nitarudi hapa na watu wa Mazingira ili kuangalia suala hilo" alisema Katibu huyo wa Itikadi 

No comments:

Post a Comment