Thursday, November 7, 2013

KIBANDA NDIYE MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI.

Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Tido Muhando (kulia) akimkabidhi tuzu Absolom Kibanda mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi 
 MHARIRI Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd. Absalom  Kibanda ameibuka mshindiwaTUZO ya uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi iliyoandaliwa na Muungano wa Klabu za waandishi wa Habari nchini (UTPC)  na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 10.

Kibanda alitangazwa leo Jijini Mwanza na Jopo la Majaji walioteuliwa kufanya mchakato wa kumtafuta mwaandishi wa Habari bora kwa mwaka huu kwenye hafla fupi katika Hoteli ya JB Belamont  na kuhudhuliwa na Wahariri wa Vyombo vya Habari, viongozi wa UTPC,Viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini , Wanahabari na Wageni mbalimbali zaidi ya 120 kutoka ndani na nje ya Tanzania'
Kibanda akinyanya juu Tuzo kuonyesha wadau na wageni waalikwa ikiwa ni ishara ya ushindi kushoto ni Rais wa UTPC Keneth Simbaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Tido Muhando.
Kibanda akifuta machozi kwa kutoamini kama ndiye amekuwa mshindi wa Tuzo hiyo.
Leila Sheikh ambaye alikuwa moja kati ya majaji akimtuliza Kibanda baada ya kumtangaza kuwa mshindi wa Tuzo.
 Huyu alishindwa kabisa kujizuia.
 Wageni mbalimbali wamehudhuria tukio hili la kwanza kabisa katika historia ya habari nchini Tanzania.
 Wanahabari wakipeperusha taarifa.
Kwa umakiiiiini...!
 Mjumbe  wa Kamati ya Majaji hao Hamza Kassongo kwa idhini ya Mwenyekiti wake Nkwabi Mwanakilala alisema kwamba Jopo la Majaji lilitembea Mikoa mbalimbali nchini kupita na kufanya utafiti kwa waandishi wa habari na wahariri wanaotekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi na kupambana na vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji kutoka kwa viongozi wa serikali, wanasiasa na makundi mbalimbali ikiwa ni lengo la kuwatisha waandishi hao.

Kassongo aliwataja majaji wengine wanne ambao walitumia muda kufanya uchambuzi wa kumpata mshindi kuwa ni pamoja na Nkwabi Mwanakilala (Mwenyekiti), Hamza Kassongo, Leila Sheikh, Dr. Ayoub Ryoba na Rosemary Mwakitwange(wote wakiwa wajumbe wa jopo la majaji ambao wametekeleza majukumu yao baada ya kuteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kufuata vigezo vilivyowekwa.
 Msemaji wa jopo hilo la Majaji hao aliongeza kuwa mshindi wa Tuzo hiyo ambaye ametangazwa amekidhi vigezo na hakuna uchakachuaji na wakubaliane na uamuzi wa jopo hilo na kisha alimwomba Leila Sheikh kupita mbele kumtangaza mshindi wa Tuzo hiyo ambapo alimtangaza Kibanda kuwa mshindi wa waandishi wa habari nchini kwa mwaka huu baada ya kushinda vigezo kumi viliyoainishwa..
 Sambamba na Tuzo pia mtunukiwa ametwaa kitita cha shilingi milioni 10 ambapo kwa mujibu wake alitamka bayana kutoa nusu ya kiasi hicho kuchangia malezi ya mjane wa marehemu Mwangosi na elimu kwa watoto wa marehemu.

Absolom Kibanda akihutubia baada ya kutangazwa huku Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan akimsikiliza kwenye Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmonte Jijini Mwanza.
Mgeni rasmi wakati wa Utoaji Tuzo hiyo, Tido Mhando alisema kwamba wanahabari sasa umefika wakati wa kukataa kutumiwa na wanasiasa na viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara kwa kukubali kupokea fedha na bahasha jambo ambalo ni hatari kwa wanahabari  pamoja na kuwadhalilisha wanahabari kwa madai ya kununuliwa na hata pengine ni kuidhalilisha taaluma nyeti inayotegemewa na jamii kupata ukweli.

“Wananchi wanatutegemea kuibua mambo mengi ya ufisadi, rushwa, wizi na hata ujangiri ikiwemo ya uhalifu na uhamiaji haramu kushika kasi ndani ya nchi yetu na hivyo waandishi kuwa majasiri kuyafichua hayo kwa kuandika ukweli na bila kupotosha umma ili jamaii inayotutegemea iweze kutuamini na kutupa ushirikiano wa dhati katika kutekeleza majukumu yetu kwa uhakika zaidi”alisema.
Aliongeza kuwa kauli za wanasiasa zinazotolewa Bungeni na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali wakati huu wa kujadiliwa Muswada wa Sheria kwa Vyombo vya Habari nchini ni dhahili kuwa lengo kubwa ni kwakandamiza waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa wananchi.

Tido alisema kuwa Tuzo kama hii ya Daud Mwangosi  Herooic Journalism Servanthood Exellence Award ni juhudi za wanahabari wenyewe kujibu maovu haya wanayotendewa na watu mbalimbali, UTPC wametuonyesha mfano na wajibu wetu leo hii, tunachowajibika kufanya ni kuwaunga mkono  ili tuzo hii iweze kuendelea kila mwaka.


Source Gsengo

No comments:

Post a Comment