Wednesday, November 6, 2013

TAKWIMU ZAONESHA ONGEZEKO LA MAKUSANYO YA KODI NCHINI

Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi ya ongezeko la thamani kwa asilimia 38 mwaka 2012/2013 kutokana na utumiaji wa mfumo mpya wa kutoa risiti kwa kutumia mashine za kielektronik na hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa mapato ya serikali.

Hayo yamebainishwa na meneja wa huduma kwa mlipa kodi Bwana Alllan Kiula wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku ya mlipa kodi ambayo yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Bwana Kiula amesema maonyesho ya mwaka huu yamekusanya wafanyabiashara mbalimbali kwa lengo la kuonyesha bidhaa zao pamoja na kuwapatia elimu juu ya utumiaji wa mashine hizo za kielektronic katika utoaji wa risiti kutokana na mauzo ya bidhaa ama huduma.

No comments:

Post a Comment