Friday, November 22, 2013

Jk awapandisha vyeo Maofisa 77 wa polisi

MO12TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWAVYOMBO VYA HABARI 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu    wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). 
Miongoni mwa maafisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ni pamoja  na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi  wa mkoa wa  Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Engelbert Kiondo, Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Ilala  ACP. Marietha Minangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP. Diwani Athumani na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela. 
Wengine ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP. Frasser Kashai, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP. Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP. David Misime, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP. Ferdinand Mtui, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP. 
Costantine Massawe, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP. Leornad Paul,  Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP. Ulrich Matei na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP. George Mwakajinga. 
Zaidi ya hao wengine ni, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Evarist Mangala, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma  Deusedit Nsimeke, Kamanada wa Polisi mkoa wa Njombe ACP. Fulugence Ngonjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari na baadhi ya  Makamanda wa vikosi, Wakuu wa vitengo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es salaam. 
Kufuatia kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao. 
Aidha, IGP Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo, na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika kuimarisha Usalama wa raia na mali zao kwa kuwa cheo ni dhamana.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment