Monday, July 1, 2013

PICHA ZA RAIS BARACK OBAMA AKIWA AMEWASILI TANZANIA LEO


Rais wa Marekani Barack Obama pamoja mkwewe wakilakiwa na mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere leo Jumatatu July 1, 2013 kwa ziara ya siku 2., kushoto ni mama Salma Kikwete.
Rais Baraka Obama akicheza ngoma alipokua akipita kwenye moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza kwa ajli ya ujio wake mara tu aliposhuka kutoka kwenye ndege ya Airforce One
Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete akitabasamu wakati mgeni wake Rais Barack Obama alipokua akitikisa mwili kwa hisia za ngoma za asili zilizokua zikitumbuizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa ujio wake leo akitokea Afrika ya Kusini.
Rais Barack Obama akiangalia moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbiza uwanjani hapo.
Rais Barack Obama akikagua majeshi ya ulinzi na usalama.
Wakina mama wamejitanda na khanga zenye picha ya Barack Obama.
Jamaa akilifagia zuria jekundu kabla ya kuwasili Rais Barack Obama. 

Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni hii ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.
Rais Barack Obama akifurahia ngoma ya kabila la Wamanda alipowasili Uwanja wa Ndege Dar es Salaam mapema leo.
ob1 ob2 ob3 ob6

No comments:

Post a Comment