Sunday, June 9, 2013

Stars ilivyo pigana Morocco,nyuma ya Ivory Coast


Mshambuliaji wa Taifa Stars Mbwana Samatta (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Morocco, Stars ilifungwa mabao 2-1.             Marakech,Morocco
TIMU ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) imeshindwa kutamba mbele ya Morocco baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1,Morocco wamepata ushindi wao wa kwanza nyumbani baada ya kufanikiwa kuhitimisha njama za kupata ushindi.
Njama za waarabu hao zilifanikiwa baada ya beki wa Stars Agray Morris kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu.
Adhabu hiyo iliweza kuifanya Stars imalize dakika 90 ikiwa na vijana tisa, Uwanjani, huku Amri Kiemba akiipata bao la kufutia machozi.
Hata hivyo Stars imebaki katika nafasi ya pili baada ya kuwa pointi 6 nyuma ya Ivory Coast yenye pointi 10 baada ya kufanikiwa kuichapa Ghambia kwa jumla ya mabao 3.0.
Morocco imefikisha pointi tano huku Ghambia ikibaki na Pointi mbili,hata hivyo Stars bado inafasi kubwa ya kusonga mbele endapo itapata ushindi katika mechi mbili zilizobaki.

Mfungaji wa bao la Stars, Amri Kiemba kushoto akimhamasisha Khamis Mcha 'Vialli' kuepeleka mpira baada ya bao wanze haraka kusaka mabao zaidi 

Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa Morocco

Samatta huyooo

Samattaaaa

Thomas Ulimwengu akifumua shuti

Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Morocco

Samatta akiwatoka mabeki wa Morocco

Samatta alifanya kazi...basi tu haikuwa bahati yake

Samatta alikuwa tishio

Kikosi cha Morocco kilichoifunga Stars 2-1

Watanzania waliokuja kuiunga mkono timu hapa

Mfungaji wa bao la Stars, Amri Kiemba akiwatoka wachezaji wa Morocco

Kikosi cha Stars leo

Salum Abubakar 'Sure Boy' akimiliki mpira pembeni ya kiungo wa Morocco

Kevin Yondan akimdhibiti mshambuliaji wa Morocco

Shomary Kapombe akimfukuza winga wa Morocco

Mbwana Samatta alikuwa anakaba pia

Zacharia Hans Poppe kulia

Aggrey Morris alitolewa kwa kadi nyekundu kwa rafu iliyosababisha penalti na bao la kwanza la Morocco

Erasto Nyoni akipambana

Mashabiki wa Tanzania

No comments:

Post a Comment