Sunday, June 9, 2013

Taifa Stars yafungwa 2-1 na wenyeji Morocco,Sasa inaweza kufufua


Taifa Stars na Morocco 1-2.
Taifa Stars jana(Juni 08,2013) ikicheza ugenini  Nchini Morocco imefungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.


Taifa Stars inayofundishwa na Kim Poulsen ilikutana na dhahama hiyo baada ya mchezaji wake Agrey Morris kutolewa nje kwa kadi nyekundu huku pia Morocco ikipata penalti dakika ya 37.


Mpaka mapumziko Morocco walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 na timu hizo ziliporudi uwanjani Morocco waliongeza bao lingine dakika ya 50 baada ya mshambuliaji wao kuwazidi mbio mabeki wa Taifa stars.


Taifa Starsna Pointi 6 sasa.
Taifa stars ikicheza pungufu ilipata bao la kufutia machozi toka kupitia kwa Amri Kiemba baada ya kuachia shuti la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Morocco.



Wakati Taifa Stars ikifungwa, wenzao Ivory Coast imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Gambia, mabao ya Ivory coast yamefungwa na Lasina Traure dakika ya 12, Wilferd Bony dakika ya 62 na Yaya Toure dakika ya 90.


Kwa matokeo hayo Ivory Coast inaongoza kundi ikiwa na pointi 10, Tanzania pointi 6, Morocco pointi 5 na Gambia wanabaki na ponti yao 1.
Wiki ijayo Stars watakuwa wenyeji wa Ivory Coast mjini Dar es Salaam na Morocco ikimenyana na Gambia.
Stars inaweza kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia ikiifunga Ivory Coast, kwani kama Tembo watafungwa na mechi ya mwisho na Tanzania ikashinda, itasonga mbele.
 



Uganda Cranes na Pointi 5 sasa.
Nayo Timu ya Taifa ya Uganda Cranes imejiweka katika nafasi nzuri  katika kufuzu kombe la Dunia  2014 baada ya kuifunga Liberia bao 1-0 katika Uwanja wa Mandela jijini kampala.


Mechi hiyo iliiisha vibaya baada ya wachezaji wa Liberia wakiongozwa na nyota wao  Roberts Omega kumzonga mwamuzi wa mchezo Adam Cordier kutoka  Chad kwa kile walichodai kuchezesha vibaya kiasi cha kuwafanya wa kushindwa kuvumulia benchi la  ufundi ilibidi wapunguze hasira ili kutuliza vurugu hizo.


Goli la ushindi liliwapa mashabiki wa Uganda hari ya juu mara baada ya  Tonny Mawejje  kufunga goli katika dakika ya sita ya mchezo, goli lililopatikana baada ya kuidanganya safu ya ulinzi ya  Liberia na kuachia shuti kali huku safu ya ulinzi  isijue cha kufanya.


Uganda kwa sasa ina pointi 5 sawa na Senegal ikiwa na pointi 6 baada ya kutoka sare ya 1-1 na  Angola huko  Luanda katika kundi  J. 


Timu inayoongoza kwa kila kundi itafuzu kwa hatua ya pili ya Makundi ya kutafuta Nchi 10 zitakazoingia hatua ya mwisho ya Mtoano ya kupata Nchi 5 zitakazotinga Brazil Mwaka 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

.



Matokeo mengine World Cup qualifiers - Africa 08 June,2013.     
     


Cape Verde         2 - 1  Equatorial Guinea

           

Sierra Leone        2 - 2  Tunisia

           

Gambia      0 - 3  Ivory Coast

           

Angola        1 - 1  Senegal

                      

Gabon        0 - 0  Congo

           

Central African Republic       0 - 3  South Africa


Uganda      1 - 0  Liberia

                      

Zambia       4 - 0  Lesotho

                      

Botswana  1 - 2  Ethiopia

           

Sudan         1 - 3  Ghana


Libya 0 - 0  Congo DR

                      

Kenya         0 - 1  Nigeria

         

           

Malawi       0 - 0  Namibia

World Cup qualifiers - Africa 


Group A

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Ethiopia431062410
2South Africa42207258
3Central African Republic410327-53
4Botswana401326-41

Group B

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Tunisia431095410
2Sierra Leone41217705
3Equatorial Guinea4112810-24
4Cape Verde410379-23

Group C

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Ivory Coast4310102810
2Tanzania42026606
3Morocco412167-15
4Gambia401329-71

Group D

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Zambia431091810
2Ghana4301142129
3Lesotho4022112-112
4Sudan4013110-91

Group E

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Congo431050510
2Gabon411214-34
3Burkina Faso31024403
4Niger310235-23

Group F

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Nigeria42204228
2Malawi41302116
3Namibia411212-14
4Kenya402213-22

Group G

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Egypt33007349
2Guinea31113304
3Mozambique302102-22
4Zimbabwe301213-21

Group H

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Algeria32018356
2Mali32014316
3Benin311134-14
4Rwanda301227-51

Group I

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Cameroon32014316
2Libya41303216
3Congo DR41212115
4Togo301225-31

Group J

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Senegal41306426
2Uganda412134-15
3Angola40403304
4Liberia411234-14

No comments:

Post a Comment