Thursday, May 9, 2013

WANAHABARI NCHINI WAASWA KUANDIKA HABARI ZINAZOKIUKA HAKI ZA BINADAMU

                                    Nikiwa pamoja na dada Vick Ntetema
           Vick Ntetema akitoa somo
                  Malima Lubasha
                              Picha ya Pamoja
               Stephen Wang'anyi akiwa na Vick Ntetema
    Augustine Mgendi akiwa pamoja na Vick Ntetema

                 Anthony Mayunga Katika harakati
                 Mtoto ambaye naye hakuwa nyuma katika kupata elimu ya utetezi wa haki za binadamu
    Wadau wakiwa katika Warsha
                        Mratibu wa THRD -Coalition Onesmo Olengurumwa
                                              Wadau wa utetezi wa haki za Binadamu


 Anthony Mayunga akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Under the same Sun Vick Ntetema


Waandishi wa habari  nchini waaswa kuandika habari za utetezi wa  haki za Binadamu,Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Under The Same Sun Vick Ntetema wakati akifungua Mafunzo ya Usalama na Tathimini ya Athari  kwa Wanachama wapya wa Shirika laa Tanzania Human Rights Defender Coalition (THRD-Coalition).

Amesema kumekuwepo na Matukio mengi ya Unyanyasaji na Ukiukwaji wa haki za Binadamu hivyo basi Waandishi wa habari wanapaswa kutumia kalamu zao katika kuibua Ukiukwaji Mkubwa wa haki za Binadamu unaofanywa hapa nchini.

Kwa Upande wake Onesmo Olengurumwa alisema kuwa  Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yatasaidia Mwanahabari kufanya kazi katika Mazingira salama kutokana na Vitendo vilivyoshamiri hivi sasa vya kuwateka Wanahabari.

Alisema Mwanahabri anapaswa kufanya kazi yake katika Mazingira ambayo yatamfanyaa awe salama Siku zote hivyo basi Mafunzo hayo yatatoa Mwanga kwa wanahabri katika utetezi lakini pia wanahabri kufanyakazi wakiwa katika Mazingira Salama.

No comments:

Post a Comment