Wednesday, May 1, 2013

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MEI MOSI UWANJA WA AMANI ZANZIBAR

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni akihutubia katika kilele cha sherehe za mei mosi
Mwakilishi wa shirila la bandari Zanzibar baada ya shirika hilo kuteuliwa kuwa shirika bora katika mashirika ya umma mwaka huu.
 
Mwakilishi wa Hospilai ya Al Rahma akipokea zawadi baada ya kuchaguliwa kuwa taasisi binafsi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani hapo uwanja wa amani mjini Zanzibar.
 (PICHA KWA HISANI YA BLOG YA VIJIMAMBO)

Na Ramadhani Ali- Maelezo Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana wa Zanzibar  wabadilike na kujenga Utamaduni wa Ujasiriamali na wawe tayari kujiajiri kupitia vyama vya ushirika vya uzalishaji mali pamoja na kuanzishsa SACCOS ili kupata mitaji yenye unafuu.

 Balozi Seif ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) zilizofanyika katika Kiwanja cha Amaan na kuwashirikisha Wafanyakazi wa Mawizara, Maidara na Mashirika ya Serikali pamoja na taasisi binafsi baada ya kuyapokea maadamano ya wafanyakazi hao.

 Amesema pamoja na Serikali kuchukua juhudi kubwa ya kupunguza tatizao la ukosefu wa ajira  kutoka asilimia saba mwaka 2007 hadi asilimia nne mwaka 2010 bado tatizo la ajira ni changamoto kubwa Zanzibar kama lilivyo nchi nyingi Duniani.

 Hata hivyo Makamu wa pili wa Rais ameahidi  kwamba Serikali itaendelea kufanya kila juhudi kupunguza ukosefu wa ajira nchini ili vijana waweze kuishi kwa amani.

 “La muhimu vijana wetu waache tabia ya kuchagua kazi.  Kazi ni kazi mradi inakupatia riziki yako kwa njia ya halali, ” amesisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
 Ameviagiza Vyama vya Wafanyakazi kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa njia ya kutoa elimu itakayowasaidia kukabiliana na ushindani wa soko la ajira la sekta binafsi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

  Amesema uzoefu unaonyesha kwamba vijana wengi  wamekosa Utamaduni wa kufanyakazi katika sekta binafsi, matokeo yake huacha kazi baada ya kipindi kifupi cha kuajiriwa na nafasi zao kuchukuliwa na vijana kutoka nchi jirani.

 Makamu wa pili wa Rais pia amevitaka vyuo vikuu nchini kuangalia mahitaji ya ajira yaliyokuwepo nchini kwa kuandaa mitaala na mafunzo yatakayowasaidia vijana kuajiriwa kwa urahisi.

 “Vyuo vyetu vikuu nchini navyo vinanafasi kubwa ya kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuandaa mitaala yao ya kufundishia na mafunzo mengine kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo kama vinavyofanya vvyuo vikuu vyengine vingi  Duniani, ”  alifahamisha Makamu wa pili wa Rais.

 Blozi Seif amewahakikishia  wafanyakazi kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuboresha maslahi yao ili kuhakikisha yanalingana na kazi wanazofanya na kwa upande wao amewataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kukuza tija  huku wakijua kwamba haki na wajibu ni watoto pacha.

 Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Shirika la kazi duniani (ILO) Bibi Hopholang Phororo ameishauri Serikali kuendelea kuwajengea wafanyakazi mazingira bora ya kazi ikiwemo kulinda afya na haki zao.

 Ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kuunga mkono  katika kusaidia juhudi za Serikali ili kuhakikisha wafanyakazi wako salama wakiwa kazini.

 Katibu Mkuu wa ZATUC Maalim Khamis Mwinyi Muhammed ameelezea kuridhishwa na mafanikio makubwa  katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa karibu sana na Shirikisho hilo na kutekeleza kanuni na sheria za kazi.

 Hata hivyo Maalim Khamis ameeleza masikitiko ya wafanyakazi wa Zanzibar kwa kutopandishwa viwango vya mishahara yao mwaka uliopita licha ya uchumi kuelezwa kuwa umekua.

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI MBEYA

8E9U2311
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi wengine kuimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa maadhimisho ya Sikuukuu ya Wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment