Sunday, May 19, 2013

BAADHI YA VIONGOZI NA WAFUSI WA CHADEMA 50 IRINGA WAKAMATWA


Hili  ni  eneo la National moto  ukiwaka katikati ya  barabara

Maeneo ya Makorongoni yakiwa yametanda  moshi mzito
POlisi wakilinda barabara  ya Iringa - Dodoma ambayo  ilitekwa na  wamachinga hao na kuchoma mataili  barabarani

Wananchi  wakiwa  juu ya nyumba  zao  kushuhudia matukio


Hali bado  yaendelea  kwenda  kombo katika Manispaa ya  Iringa  baada  ya  askari  polisi kukamata  watu  zaidi ya 50 akiwemo  aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Mvinjini Abuu Majeck

Hadi  sasa biashara  katika mji mzima  zimesimama na polisi  wameendelea kuweka  sawa  ulinzi katika mitaa mbali mbali .

Kwa  sasa baadhi ya mitaa ya mji  wa Iringa imetanda  moshi  uliotokana na mataili  yaliyochomwa na machinga  hao.

Taarifa  za  sasa  kutoka jeshi la  polisi ni kwamba mbunge  wa  jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae anadaiwa  kuwa chanzo cha vurugu  hizo anasakwa  japo mtandao  huu nusu saa iliyopita  ulimshuhudia akiwa  eneo la chuo  cha Tumaini katika harambee  inayoendeshwa na waziri mkuu  wa zamani Mh. Sumaye

Nipo  njiani kuelekea  Tumaini niliko mwacha  mbunge Msigwa  undani  wa ukweli  wa mambo utaupata  hapa  endelea  kutembelea...... 


sc Francis Godwin

No comments:

Post a Comment