Monday, May 20, 2013

MAMLAKA YAPEWA SIKU 21 KUTOA TAKA MAENEO YA WAZI.

Serengeti
 
-MADHARA ya kutoa  zabuni kwa kampuni zisizo na uwezo yameanza kujionyesha katika Mamlaka ya Mji wa Mugumu wilayani Serengeti,kufuatia Kampuni ya Ujenzi Youth Group iliyopewa zabuni ya kuzoa taka kushindwa na kupelekea mji kuzaa taka ,hali inayoibua hofu ya magonjwa ya mlipuko.
Kampuni hiyo ilipewa zabuni hiyo kwa malipo ya sh,milioni 48 kwa mwaka wakati haina vifaa vya kufanya kazi hiyo,na kuacha kampuni nyingine iliyoomba kwa sh,mil.38 ikiwa na vifaa vya kuweka mji huo unaotarajiwa kuwa kitovu cha utalii safi.
Mtendaji wa Mamlaka hiyo Gedioni Obel mbele ya baraza la madiwani halmashauri ya wilaya hiyo lililotaka  maelezo kutokana na viwanja vya wazi kugeuzwa madampo ikiwa ni karibu na nyumba za kulala wageni,alikiri kuwa mzabuni huyo hana uwezo na ndiyo chanzo cha kuzagaa kwa taka.
Hata hivyo maelezo yake yaliibua maswali kutoka kwa madiwani waliotaka kujua sababu za kumchukua mzabuni asiye na uwezo wala vifaa kufanya kazi hiyo kwa gharama ya juu na kumwacha aliyeomba kwa gharama za chini   akiwa na uwezo wa kuweka mji safi.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jumanne Kwiro alisema hali hiyo haiwezi kuvumiliwa kwa kuwa inapingana na jitihada wanazofanya za wilaya hiyo kuwa kitovu cha utalii.
“Inasikitisha sana mji kuwa mchafu namna hii,maeneo yote ya wazi yamegeuzwa dampo kwa madai kuwa ni sehemu ya kukusanyia ….mbona hazitolewi zinakaa hadi wiki…ni mtalii gani atakuja mji huu na kulala hoteli akivuta hewa chafu….tunatoa siku 21 taka zote ziwe zimeondolewa”alisema na kuungwa mkono na madiwani wenzake.
Pia waliutaka uongozi wa  hospitali ya Nyerere ddh kuhakikisha wanajenga choo kipya kunusuru afya za wagonjwa wanaopata huduma  hapo kutokana na kilichopo kujaa .
Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Goody Pamba alikiri kuwepo na tatizo hilo la uchafu kuzagaa mji wa Mugumu na wakati mwingine kukaa muda mrefu bila kuzolewa na kuelezea kuwa linashughulikiwa ili kuhakikisha mji unakuwa msafi kwa kutumia sheria ndogo ndogo .
Mwisho.
 MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU SERENGETI IMEWEKA DAMPO LA TAKA KATIKA UWANJA WA MICHEZO NATIONAL HOUSING,IKIWA NI KARIBU NA MAKAZI ,BARABARA INAYOPITISHA WAGENI WA NDANI NANJE YA NCHI,VIONGOZI WOTE WA WILAYA
 TAKA HIZO HUKAA KWA MUDA MREFU BILA KUTOLEWA KWA KILE KILICHODAIWA NA WATENDAJI WA MAMLAKA HIYO KUWA MZABUNI ALIYEPEWA TENDA HIYO KWA SH,MIL,42 KWA MWAKA HANA UWEZO WALA VIFAA,LAKINI BODI YA ZABUNI ILIMWACHA ALIYEOMBA KWA SH,MIL.38 AKIWA NA VIFAA NA KUMPA ASIYE NA VIFAA.
 WATOTO WANAOCHEZEA KATIKA VIWANJA HIVI WAKO HATARINI KIAFYA.
 DAMPO LINGINE LIMEWEKWA KARIBU NA NYUMBA YA KULALA WAGENI YA GESASE,IKIWA NI KARIBU NA NYUMBA ZA NHC KUKAKO KAA VIONGOZI WA HALMASHAURI HIYO,IKIWEMO AFISA AFYA WA MAMLAKA HIYO.
 NYUMBA ZINAZOONEKANA MBELE YA DAMPO HILO NI MAKAZI YA MAAFISA WA SERIKALI AMBAO WAMERUHUSU DAMPO HILO KUWEPO HAPO.
LICHA YA TAMBO ZA VIONGOZI WA KISIASA KUWA MJI HUO WANATAKA UWE KITOVU CHA UTALII,MAENEO YOTE YAWAZI YAMEGEUKA KUWA MAJALALA YA TAKA ,

No comments:

Post a Comment