Sunday, April 14, 2013

YANGA WAFURAHI KILELENI, AZAM YAKABWA KOO, YALAZIMISHA SARE YA 2-2 NA MNYAMA TAIFA!

azam vs simba
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam

Hatimaye ubishi wa timu za Azam Fc wana lambalamba na wekundu wa msimbazi Simba umemalizika leo hii uwanja wa taifa baada ya kuchoshana nguvu kwa kufungana sare ya 2-2.

Matokeo hayo, yanaiongezea Azam pointi moja na kufikisha 47 kibindoni  ikibaki nafasi ya pili, nyuma ya Vinara Yanga wenye pointi 52, wakati Simba wanasalia nafasi ya nne kwa pointi zake 36, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37 nafasi ya tatu.

Hadi kipindi cha kwanza cha kipute hicho kulichochezeshwa na mwamuzi Orden Mbaga kinamaliziaka, Mnayama alikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Nyota na Chipukizi wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ alifunga mabao yote mawili kwa upande wa klabu yake akiunganisha pasi nzuri za winga mwenye kasi Mrisho Khalfani Ngasa aliyeaambaa na gozi wingi ya kushoto.

Kipre Tchetche aliifungia Azam kwa penalti dakika ya 29, baada ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kuangushwa kwenye eneo la hatari na William Lucian ‘Gallas’.

Refa Orden Mbaga alimpandisha jukwaani kocha Muingereza wa Azam, Stewart Hall dakika ya 31 kwa kutoa maneno machafu, akilalaimikia uchezeshaji wa refa huyo.

Kipindi cha pili, Azam walirejea kwa nguvu na kutaka kujinusuru na kipigo na walitimiza ndoto yao baada ya  Humphrey Mieno kuunganisha shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na kiungo Khamis Mcha ‘Vialli`’katika dakika ya 72 na kuzamisha gozi nyavuni..

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Afisa habari wa klabu ya Azam Fc Jafar Idd Maganga amesema wamepokea matokeo kwa mikono miwili kwani ndio soka hilo.

Idd alisema “Tulisema tangu awali kuwa simba ni wazuri na tulikuwa tayari kupokea matokeo yoyote yale, tumetoa sare nao lakini tunajipanga kwa mechi zijazo”.

Kwa uapnde wa simba kupitia kwa kocha msaidizi Jamhuri Kiwhelu Julio alisema bado wanahitaji kupata muda wa kutosha kwani ndio kwanza timu inaanza kushika kasi.

“Wana Simba tuwe na umoja, timu imecheza vizuri na tunamshukuru mungu kwa kupata pointi moja na kwa pamoja tunatakiwa kusonga mbele”. Alisema Julio.

kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Haroun Chanongo/Edward Christopher, Abdallah Seseme, William Lucian/Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho Ngassa/Fliex Sunzu.

Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Luckson Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk, Salum Abubakar, John Bocco/Abdi Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na Kipre Tchetche

No comments:

Post a Comment