Monday, April 29, 2013

WATU WATATU WAUAWA MKOANI MARA AKIWEMO MMOJA KUCHINJWA NA KUTENGANISHA SHINGO NA KIWILIWILI
Watu wawili wamekufa katika Matukio tofauti Manispaa ya Musoma Mkoani Mara,taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa Waandishi wa habari imeeleza kuwa tukio la Kwanza Mtu mmoja mwendesha Pikipiki ameokotwa akiwa amekufa katika eneo la Rwamlimi Manispaa ya Musoma mkoani hapa.

Taarifa ya tukio hilo inaeleza kuwa Marehemu aliyekuwa anafahamika kwa jina la Maendeleo Yohana umri miaka 45 aliokotwa huku Miguu na Mikono yake ikiwa imefungwa Kamba.Mnamo April 27 majira ya saa mbili usiku Marehemu  aliitwa na Mteja kwenda mahali alikofia.

Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kutokana na tukio hilo,wakati huo huo taarifa hiyo imeeleza kuwa Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Regina Manyama miaka 67 amechinjwa hadi kutengenisha shingo na Kiwiliwili na watu wasiojulikana.

Katika tukio la tatu taarifa hiyo inaeleza kuwa Binti mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na asiyefahamika kwa majina,kabila wala Makazi amekutwa amekufa katika eneo la Mgaranjabo Manispaa ya Musoma mkoani Mara na maiti yake kuharibika huku Maiti yake ikiwa pembeni ya mfereji wa maji jirani na eneo la kuchimbia mchanga.  

Mwili wa marehemu huyo umekutwa ukiwa uchi na chanzo cha kifo kinachunguzwa ambapo mpaka sasa hakuna anayeshikiliwa na jeshi hilo.

Kufuatia Matukio hayo ya Mauaji,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ameoa wito kwa wananchi huku akihimiza wenye taarifa za siri kuzitoa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria

No comments:

Post a Comment