Thursday, April 25, 2013

MTENDAJI,MKANDARASI WAGUSHI NA KUIBA SH.MIL.10 ZA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA MONUNA

Serengeti.
 
OFISA Mtendaji kijiji cha Monuna  kata ya Nyambureti Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Juma Ntora kwa kushirikiana na Kampuni ya J.N.L. Construction and General Traders Ltd ya Musoma  wanadaiwa kughushi nyaraka na kuiba sh.mil.10 za ujenzi wanyumba ya waganga  Zahanati ya kijiji  hicho.
 
Mradi huo ulipata sh.34,895.295.00 kupitia Mpango wa MMAM na ziliwekwa benki ya NMB Tawi la Mugumu julai 31,2012 kwenye akaunti ya mradi wa zahanati namba 3026600268,waeka sahihi wakiwa ni wajumbe wawili na ofisa mtendaji huyo.
 
Wizi huo imebainika ulifanyika septemba 21,2012 ambapo badala ya kuchukua sh.7,890,000=zilizopitishwa na kamati ya ujenzi wa nyumba ya mganga Monuna ,na kuridhiwa na  aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Kimulika Galikunga kwa sasa yuko Mpanda,lakini wakaongeza namba  moja mbele na kusomeka 17,890,000.
 
Blogu ilibaini muhtasari wa kamati uliandaliwa na ofisa mtendaji huyo agosti 20,2012 badala ya kamati ya ujenzi ,lakini uliwekwa sahihi na Juma Kongo(Mwenyekiti)Mussa Nyandete(Katibu)Meshack O.Janes(Mjumbe)Christina Maro(mjumbe) na John Apiyo Agar(mjumbe).
 
Muhtasari huo ulioambatanishwa na barua yenye kumb.NoK/U/K/M./VOL10/012 unaonyesha kiwango kilichotakiwa kuchukuliwa ni 7,890,000= baada ya  mhandisi wa halmashauri hiyo Mokoro Magori ,Katibu wa afya Peter Shilingi  kwa niaba ya Mganga mkuu wa wilaya na aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji Galikunga kupitisha  hati ya ukaguzi hatua ya kwanza.
 
Hati hiyo Kandarasi namba LGA/063/2008-2009/8/MMAM/09 inaonyesha mkandarasi JNL.Construction and General Traders Ltd, ilisainiwa tarehe kati ya 13-17/9/2012,inatofautiana na mhitasari na barua ya kuchukua fedha ambao uliandaliwa tarehe 20,8,2012.
Malipo hayo yakiwa ni kwa ajili ya shughuli za awali za msingi,kumwaga zege la jamvi ya nyumba hiyo ya watumishi wawili wa afya.
 
Uchunguzi wa blogu hii ulibaini kuwa wizi huo ulifanikiwa kirahisi baada ya kuongeza tarakimu moja mbele baada ya kuwa mtendaji huyo ameacha nafasi wazi,pia kwa kutumia  jina la Solomon Eliud Nkaina toka kwenye muhtasari badala ya jina la Kampuni hali ambayo inaashiria kuwa wanakwepa mapato ya serikali kwa kutokutumia jina la kampuni.
 
Mweka sahihi.
Mjumbe na mweka sahihi kamati ya ujenzi wa nyumba hiyo Meshack Janes alisema wizi huo aliubani wakati alipokwenda Benki ya NMB tawi la Mugumu kuangalia salio na kubaini kati ya fedha walizoidhinisha milioni 10 ziliibwa.
 
“Nilipitia hapo NMB benki baada ya kutoka benki ya CRDB kupokea malipo yangu ya tumbaku…kwa kuwa mimi ni mweka sahihi nikaona ni vema kuchukua salio kwa kuwa tulishakubaliana tukifika mjini tupate muda wa kuhakiki na kutoa taarifa kwenye kamati”alisema.
 
Kuhusu wizi huo alisema ulianzia kwenye muhtasari aliouandaa na baada ya kuambiwa urekebishwe alitumia sahihi za wajumbe za awali na kisha kuandaa muhtasari mwingine bila kuwashirikisha na kwenda kuchota fedha hizo.
 
Mtendaji.
 
Alipotafutwa kwa njia ya Simu Ofisa mtendaji Juma Ntora alikiri kuwepo kwa tatizo na kuwa tayari anahojiwa”ninahojiwa an PCCB  kwa sasa kuhusiana na suala hilo”alisema .
 
Alikiri kushirikiana na mwakilishi wa kampuni kupora fedha hizo,”hata hivyo jamaaa amekimbia na kuniachia mzigo,nimekubali kulipa hizo mil.10 zote ili mambo yaishe,maana hata pesa hizo sikufanikiwa kupata mgao.
 
Kampuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya ya JNL Construction and General Traders Ltd  Lameck Chacha alikiri mfanyakazi wake kuhusika na wizi huo,”niliambiwa nikafuatilia ni kweli alishirikiana na mtendaji akamwandikia kwa jina lake badala ya kampuni ,ni wizi huo na alitoroka sijui alipo”alisema.
 
Hata hivyo alikiri kuwa hakuna sehemu aliyotoa taarifa kuhusu mfanyakazi wake kuiba na kutoroka,kwa madai kuwa yeye anajua fedha walizokubaliana na kijiji zipo na akimaliza kazi atalipwa kama walivyokubaliana.
 
Serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Damas Kongo Watanda alisema ,suala hilo wanategemea vyombo husika kuchukua hatua kwa kuwa wizi huo unaathari kubwa kwa jamii,”akina mama wanatembea zaidi ya kilometa 10 kupata huduma”alisema.
 
Ofisi ya Ded/Dc.
Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na Mkuu wa wilaya imetaarifiwa na kuwa suala hilo limeishaelekezwa PCCB kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua hatua kwa wahusika.

No comments:

Post a Comment