Thursday, April 25, 2013

MIKONONI MWA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA KUKU,MWINGINE ASHIKILIWA KWA KUMCHOMA MTOTO SEHEMU ZA SIRI

  MWANAUME mmoja mkazi wa kata ya Kigera katika Manispaa ya Musoma aliyefahamika kwa jina la Yusufu Bakari (28) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara kwa kosa la kufanya mapenzi na kuku na kumsababishia maumivu makubwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,kamanda wa Polisi mkoani Mara Absalom Mwakyoma alisema tukio hilo lisilo la kistarabu lilitokea aprili 24 majira ya saa tatu asubuhi katika maeneo ya Kigera katika nyumba ya mama Nyamela Kitambara (76)

Alisema siku ya tukio mtuhumiwa wa kosa hilo ambaye ni mpangaji katika nyumba hiyo alimchukua kuku wa mama mwenye nyumba na kuingia nae ndani na kuanza kufanya mapenzi na kuku huyo hali iliyomfanya mama huyo kupiga kelele baada ya kuona tukio hilo likifanyika.

Kamanda Mwakyoma alisema  baada ya mama huyo kupiga kelele majirani walikusanyika katika nyumba hiyo na kuanza kumshambulia kwa kipigo mtuhumiwa wa tukio hilo na kumsababishia maumivu makali ambapo baadae alifikishwa mikononi mwa jeshi la polisi huku kuku huyo akiwa amepelekwa katika ofisi ya Afisa Mifugo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Katika tukio lingine,Mwakyoma alisema Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabethi Bureko (26) mkazi wa kata ya Nyamatare Manispaa ya Musoma anashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kumchoma moto mdomoni na sehemu za siri mtoto wa miaka  (8) Robhi Marwa na kumsababishia maumivu makali.

Chanzo cha kuchomwa moto mtoto huyo ni pale alipokutwa na mama huyo akimnywesha uji mtoto wake wa miaka 2 huku akiendelea kulia na kudai mlezi alikuwa akinywa uji wa mtoto ndipo alipochukua kibatari na kuanza kumchoma katika maeneo hayo.

Kamanda Mwakyoma alidai baada ya majirani kupata taarifa za tukio hilo walimfata mtuhumiwa na kuanza kumshambulia kwa kipigo na kumsababishia maumivu makali na kupelekea kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara huku akiwa katika ulinzi wa jeshi la polisi.

Kufuatia matukio yote mawili,Mwakyoma alisema mtu yoyote kabla ya kufanya jambo lolote inabidi kuishughulisha akili kutambua kila anachotaka kukifanya kwani kuna matukio mengine yanadhalilisha na kumtoa mtu katika ubinadamu.

"Ndugu Waandishi matukio kama haya mtu inatokea anayafanya bila kuchukua muda wa kuishughulisha akili kabla ya kufanya maana kitendo cha kumchoma mtoto wa miaka 8 mdomo na sehemu zake za siri ni kitendo cha kinyama na inashangaza kufanywa na mtu mwenye akili zake timamu.

"Watu inatakiwa kubadilika na kuacha kujichukulia maamuzi ambayo baadae inakufanya kuijutia nafsi,mwingine akiwa na aikili zake timamu anakwenda kufanya mapenzi na kuku hizi akili gani...kwa kweli tunaitaka jamii kutafakari kwanza kabla ya kufanya jambo lolote,alisema Mwakyoma.

No comments:

Post a Comment