Waziri
wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari
katika bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye viwanja vya
Leaders Kinondoni jijini Dar es salaal leo, ambapo kumefanyika michezo
mbalimbali kwa timu shiriki zikitoka katika vyombo mbalimbali vya
habari, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa kama mgeni rasmi amegawa nishani na
vikombe kwa washindi wa bonanza hili linaloandaliwa na chama cha
waandishi wa habari za michezo TASWA, Katika hotuba yake kwa wanahabari
Mwakyembe amesema kama kila mtu atataka kugombea uras nani atafanya
kazi nyingine? Akaongeza kuwa yeye anajikita zaidi kufanya kazi zake
katika wizara anayoitumikia ya Uchukuzi ili kuwatukia watanzania
Waziri
Mwakyembe akimvisha nishani mmoja wa wachezaji wakati alipotoa zawadi
kwa washindi kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando na Mkuu wa
Uhusiano na Sheria TBL Bw. Steven Kilindo
Mchezaji
wa Bloggers FC Muhidin Sufiani akibebwa juujuu mara baada ya kupachika
penati na kifungia timu yake wakati zilipopambana na timu ya chuo cha
DSJ na Bloggers FC kushinda kwa penati 3-2
Golikipa
wa timu ya Bloggers FC Othman Michuzi akinyanyuliwa na mchezaji
mwenzake Mroki Mroki mara baada ya timu hiyo kuifunga timu ya DSJ penati
3-2
Kikosi cha Bloggers FC kikiwa katika picha ya pamoja Wangenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakiwa katika
Kiongozi
wa kundi la Taarab la Jahazi Mzee Yusuf akiwarusha waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali katika bonanza lililofanyika kwenye viwanja vya
Leaders jijini Dar es salaam Waandishi wa habari wakidibwilika stejini
Blogger
John Bukuku wa Fullshangweblog akiwa na Blogger wa Sufianimafotoblog
Muhidini Sufiani ambaye pia anaweza UDJ kama anavyoonekana hapa
Mchezaji wa Bloggers FC Majuto Omary akimiliki mpira wakati wa mchezo wao na timu ya SIBUKA Othman Michuzi akijiandaa kudaka mpira wakati wa mchezo kati ya Bloggers FC na DSJ ambapo Bloggers imeshinda penati 3-2 Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakionyesha uwezo wao
Waziri
wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiwasili katika viwanja vya Leaders
katika bonanza la waandishi wa habari linaloandaliwa na TASWA Kulia ni
Mkuu wa Uhusiano na Sheria TBL Bw. Steven Kilindo na kushoto ni
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Juma Pint
No comments:
Post a Comment