Sunday, April 21, 2013

ABDURAHMAN KINANA AWAAMBIA WABUNGE WA CCM TEMBEENI KIFUA MBELE NA KUKOSOA MAOVU YA SERIKALI, CHADEMA WAMESHINDWA KAZI

k1 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM  Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya Kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro mjini , mkutano huo ukikuwa ni wa kumalizia  ziara yake ya siku kumi katika wilaya zote za mkoa wa Morogoro ambapo amehutubua taifa moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni  ya Shirika la Utangazaji la taifa  TBC. Kinana amezungumza mambo mengi akiwaambia wabunge wa CCM kutembea kifua mbele na kukosoa waziwazi uozo wowote utakaofanywa na viongozi wa Serikali na Chama kwani CCM ndiyo wenye kusema na kukosoa makosa ya kiutendaji katika serikali kwasababu  ndiyo iliyoaminiwa na watanzania kuongoza watanzania, CHADEMA wameshindwa kazi ndiyo maana wanafanya fujo bungeni na kujaribu kuvuruga kizuri chochote ambacho serikali ya CCM inataka kufanya kwa maslahi ya watanzania
  k4 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Diana Salum mkazi wa Kata ya Kilongo Manispaa ya Morogoro baada ya kuzindua moja ya visima 23 virefu vya maji vilivyochimbwa na mbunge wa jimbo hilo Mohammed Aziz Abood,2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akifungua bomba la maji mara baada ya kuzindua kisima hicho leo. 3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kisima cha maji katika kata ya Kilongo Manispaa ya Morogoro, kulia ni Mohammed Aziz Abood Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini na kushoto ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro 5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Kata ya Kilongo. 6Moja wa visima vya maji vilivozinduliwa leo hiki ni cha kata ya Kilongo 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Kilongo kushoto ni Mbunge wa Morogoro Mjini Mohammed Aziz Abood 8wananchi wakiwa wamekusanyika kushuhudia uzinduzi huo. 9 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akifungua bomba la maji mara baada ya kufungua kisima cha maji katika kata ya Kichangani, kulia ni Mbunge wa Morogoro Mjini Mohammed Aziz Abood.

No comments:

Post a Comment