Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP),
walinunua jengo la ofisi hii kutoka kwa
Mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani
Benki ya Rasilimali ya Tanzania mnamo tarehe 15th June, 1997.
Wapangaji wasiohalali walikwenda mahakamani
wakiwashitaki Benki ya Rasilimali ya Tanzania pamoja na TGNP na kesi
ilifunguliwa tarehe 16th July 1997 kesi ilipewa Na. 215/1997. Madai
ya washitaki yalikuwa yafutayo:
a)
TGNP ilipendelewa katika mchakato mzima wa tenda ya
manunuzi ya jengo hili na kwamba TGNP hawakuwa wazawa.
b)
Utoaji wa tenda kwa upande wa Beki ya Rasilimali
Tanzania ulikuwa batili kwa sababu haukufuata/haukuzingatia sheria ya nchi ya
manunuzi na hivyo kukiuka haki za kimsimgi (failure to observe the law, public
policy and the rules of natural justices)
TGNP kama washitakiwa
walishinda kesi hiyo ya madai namba
215/1997 iliyofunguliwa na waliokuwa wapangaji. Jengo lenye kesi ni jengo la
gorofa moja zilipo Ofisi za Makao Makuu ya Shirika Mabibo Dar es salaam.
Chini ya Mhe. Jaji T.B.
Mihayo, 15 Oktoba 2009, TGNP Ilishinda kesi hiyo na walalamikaji walidai kuwa
TGNP imependelewa. Oktoba 19, 2009, walifungua rufaa katika makahakama kuu ya
Rufaa ya Tanzania, wakiipinga hukumu ya kesi ya msngi namba 215/1997 na kukawa
na kesi ya rufaa namba 129/2009 ili pia waendelee kukaa kwenye jesngo hilo.
TGNP iliiomba mahakama
kufuta ombi la walalamikaji la kuendelea kuwa kwenye jengo ili shirika liweze
kufanya shughuli zake, kesi ambayo ilisikilizwa na majaji watatu waheshimiwa
jaji Msasali, jaji Msofe, na jaji Rutakanga Julai 22,2011.
Tarehe 23. 08.2011,
TGNP iliamua kwa mujibu wa sheria kuwatoa kwa nguvu wapangaji hao ambao kwa
muda wote wa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye jengo la
TGNP bila kulipa kodi wala ruhusa yao, lakini siku chache baadaye walirudi.
Pamoja na ushindi walioupta TGNP bado waliendelea kuheshimu maamuzi ya mahakama
kutokana na shauri walilolipeleka mahakamani.
Mwaka 2012 walalamikaji walienda tena Mahakama Kuu
wakiomba kurekebisha majina ya watu waliosomewa hukumu kuwa watu wengine walio hukumiwa hawakuwa sehemu
ya kesi hii!! TGNP tuliona kuwa hii
ni mbinu tuu ya kuchelewesha kesi ambayo imekuwa ikitumika kwa miaka mingi. Jaji Mwaikugile aliikubali
hiyo barua akitaka wakaandike vizuri zaidi ili hoja yao isikilizwe. Kesi hii
imepangiwa kusikilizwa tena hapo tarehe 26 Februari 2013, lakini hadi tarehe
08.03.2013 hawakuwa wamewasilisha na leo tarehe 13.03.2013 jaji ametupilia
mbali ombi lao.
Kesi hii imekuwa ni changamoto kwa TGNP, huu ni
mwaka wa 16 tangu shirika linunue jengo hili.
Sote kwa pamoja
tunaamini katika haki na na rasilimali lazima zirudi kwa wananachi!
Imetolewa na
Imetolewa na:
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji
TGNP
No comments:
Post a Comment