Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama, wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza
ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Gabriel Tupa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi, wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza
ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati
walipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza
ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Gabriel Tupa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
***********************************
MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MARA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jumapili Februari 3, 2013
ameanza rasmi ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Mara.
Akiwa
Mkoani Mara Mhe. Makamu wa Rais, anatarajia kukagua shughuli mbalimbali
za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kufungua Barabara inayounganisha Mkoa
mpya wa Simiyu na Mkoa wa Mara.
Aidha
Makamu wa Rais, atazindua rasmi Kivuko cha Mv. Musoma, kinachofanya
kazi ya kusafirisha wananchi ambao ni wakazi wa Rorya na Musoma, ambapo
pia atazindua mradi wa nyumba za Watumishi wa Umma, mkoani Mara na
kuzungumza na wananchi kabla ya kuondoka kurejea jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment