Wednesday, March 6, 2013

MAKAMU WA RAIS AZINUA KIVUKO CHA MV MUSOMA


1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko cha MV Musoma, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara. Kutoka (kulia) kwake ni mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, John….Picha na OMR
3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa Kivuko cha Mv Musoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013, kijiji cha Kinesi Wilayani Rorya. Picha na OMR
5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Chama na Serikali, wakati akitoka kukagua Kivuko cha Mv. Musoma, baada ya kukizindua rasmi leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi wilayani Rorya. Picha na OMR
4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakiwa ndani ya Kivuko cha Mv. Musoma baada ya kuzinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais, leo Feb 5, 2013 wilayani Rorya kijiji cha Kinesi mkoa wa Mara. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment