Sunday, February 24, 2013

WANAHABARI 150 WANUSURIKA KUTEKWA KWA KUDODOSA GESI MTWARA


Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara, wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na  mabasi madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo kupeleleza suala la Gesi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

 Na Richard Mwaikenda, Mtwara

WAANDISHI wa Habari 150  kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.

Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.

Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akizungumza wakati wa kufungua rasmi hafla hiyo, alitangaza kuwa Mkuu wa Mkoa Simbakali hatutakuwa naye amepata dharula ameondoka. Wengi wa wageni waalikwa kwa wakati huo hawakujua ni dharula gani.

Baada ya muda wakati hafla hiyo ikiendelea baaddhi ya waalikwa walipata taarifa ya mpango huo wa wananchi wa kuwadhuru wanahabari, na kwamba Kamati ya Usalama ya mkoa huo ilikuwa inaendelea na kikao cha kuwanusuru wanahabari hao walikuwa zaidi ya 140.

Ndipo mmoja wa watumishi wa NHIF, akawaeleza kwa siri baadhi ya wanahabari kuwa waambiwe na wengine kwamba badala ya kuondoka saa mbili asubuhi, safari itakuwa saa 11 alfajiri na wote walitakiwa kukusanywa na magari mahotelini na kwenda kukutana ofisi ya NHIF za mkoa huo.

Mwandishi wa habari wa gazeti hili ambaye alikuwa miongoni mwa wanahabari hao, anasema jambo hilo la kutisha liliwafanya wengi wao kuwa na hofu.

Anasema ilipofika muda wanahabari hao walisafirishwa kwa mabasi madogo matatu aina ya Coaster kwenda Lindi huku msafara huo ukilindwa na watu wa usalama.

Walipofika eneo la Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),  nje kidogo ya Mji wa Lindi, walikuta askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa tayari kuwalinda huku wakiwa na silaha.

Wanahabari kuona hivyo walifurahi na kushuka kwenye magari huku wengi wakienda kuwaslimia askari hao pamoja na kupigapicha nao, wakisubiri mabasi makubwa ya kuwapeleka Dar es Salaam.

Akielezea mmoja wa wanahabari hao sababu za wananchi kuwahisi kuwa wamekwenda kupeleleza suala la Gesi, ni kutokana na kitendo cha baadhi yao kwenda mitaani kuwahoji wananchi jinsi hali ilivyo kwa sasa baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuumaliza mgogoro wa kusafirisha Gesi  kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Alisema kuwa baada ya wananchi hao kuhojiwa, walianza kuwasiliana kjwa simu na wananchi wenzao na kuanza kupanga mikakati ya kuwadhuru kwa kuyazingira mabasi watakayopanda asubuhi yake kwenda Dar es Salaam.

Ilipotimu saa nne asubuhi mabasi yaliingia eneo la Veta Lindi huku yakiwa na baadhi ya wanahabari waliochelewa kuamka alfajiri. Wanahabari hao walipanda kwenye mabasi hayo huku baadhi ya magari mengi yaliyokuwa na FFU yakiendelea kulinda msafara huo.

MOVIE MPYA YA STIVE YAANZA NA GUNDU ASWEKWA LUPANGO MABATINI

 Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.Kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog

Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.

Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.

Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 

Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.

Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.

Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
 Eneo la tukio la ajali hiyo.
 Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
 Kushoto ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
 Huu ndiyo waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
 Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
 Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
 Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
 Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
 
source Kamanda wa Matukio

No comments:

Post a Comment