Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali inayojishughulisha na
uendelezaji wa wajasiriamali vijana Tanzania Bara( YESI) Bw. Denis Maira
(kushoto) akiongeza na waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam juu
ya kongamano linatarajia kuwakutanisha wajasiriamali vijana 250
ambalo litaanza tarehe 6 hadi 8 Mwezi huu . Kongamano hilo linatarajiwa
kugharimu shilingi milioni 15 .Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Benki ya NBC
Eddie Mhina.
……………………………………………………
Na Heka Paul na Shakila Galus – MAELEZO_Dar es ssalam
Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali
inayojishughulisha na maendeleo ya Vijana (Young Entrepreneurs Support
Initiatives –YESI) inatarajiwa kuendesha kongamano la vijana linalolenga
kuwahamasisha kujiajiri katika ujasiriamaliili kukuza biashara nchini.
Akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam
Mwenyekiti Mtendaji Denis Maira , alisema kuwa kongamano hilo
liwashirikisha vijana 250 wa mjini hapa na linatarajiwa kugharimu
shilingi milioni 15 .
Alisema kuwa kongamano hilo pia litatoa fursa kwa kwa vijana
kujifunza mbinu za kukuza biashara na kutengeneza ajira kwa vijana
wenzao.
Maira aliongeza kuwa kongamano hilo la siku mbili
litawakutanisha wadau wa sekta ya ujasiriamali mbalimbali ambao
watajadiliana mbinu za kufungua milango ya maendeleo endelevu ambayo
itawawezesha vijana wengi kupambana na tatizo la ajira kwa kujiingiza
katika ujasiriamali .
“Hili ni kongamano la kitaifa ambalo linalenga kutafuta
suluhisho ya changamoto zinazowakabili vijana hasa tatizo sugu la ajira
na athari zake kiuchumi na kiusalama” alisema Maira.
Alisema kuwa hatua itawasaidia vijana katika harakati za
kupambana na umaskini na hivyo kujipatia kipato na kuendeleza taifa kwa
ujumla.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kongamano hilo litatoa fursa kwa
vijana watakaohudhuria kujifunza jinsi vijana wa Kitanzania ambao ni
wajasiriamali waliofanikiwa kuanzisha na kukuza biashara zao na hatimaye
wakatoa ajira kwa watanzania wengine wakiwamo vijana.
Vilevile washiriki watapata fursa ya kubainisha fursa
mbalimbali za kijasirimali , masoko ya ndani na nje na jinsi ya kupata
mikopo ya kuwawezesha.
No comments:
Post a Comment