Bi Annastazia akiwa Katika Kitanda cha Hospital ya Mkoa wa Mara
Hapa nikimkabidhi mama yake Annastazia sh 10,000 iliyokuwa imetumwa na mamaAbduwel
Natumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote walioguswa na Ugonjwa wa Bi Annastazia ambaye amekuwa akisumbuliwa
na Kuvimba kwa Mguu wake wa Kushoto,kuna watu mbalimbali ambao walipiga simu
wakielezea kuguswa na hali hiyo lakini wapo wengine walioenda mbali zaidi na
kutoa pesa kidogo ambazo zitaweza kumsaidia
Bi Annastazia.
Mpaka sasa tayri kuna watanzania wawili ambao
wametoa fedha ambazo kwanjia moja
zitamsaidia Bi Annastazia,kwa vile nilitumia mtandao huu kuwaomba wamsaidie pia
napenda kutumia mtandao huu kutoa shukrani lakini pia kuwaomba wengine ambao
hawajafanya hivyo kumsaidia Bi Annastazia.
Waliotoa ni pamoja na
1.
Mama Abduweli wa Mamlaka
ya banadari Dar es Salaama- Sh 10,000
2.
Dada Edna Lwanji kutoka nchini Uingereza
–Sh 137,555.30
Pamoja na kupokea fedha hizo leo nimeongea na mama
yake Annastazia na kusema kuwa Mtoto wake anatakiwa kupelekwa jijini Mwanza
kwaajili ya kukatwa mguu huo kutokana na vpimo vilivyopatikana baada ya kupigwa
X ray.
Hivyo basi watanzania
tuendelee kumsaidia Annastazia kwani Mpaka sasa Mama yake hana fedha na hana
msaada wowote kwani ni Mjane ,kama utahitaji kumsaidia Bi Annastazia kutuma kwa
M Pesa katika namba 0756 035 825
No comments:
Post a Comment