Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Mahakama ya Wilaya Kongwa Jana ilimuhukumu Bw. Jumanne Hassan Miaka (22) mkazi ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Liganga, Kata ya Chitego tarafa ya Nzoisa wilayani humo
kutumikia kifungo cha miaka (30 ) jela na kuchapwa viboko (12) baada ya
kumtia hatiani kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la tano.
Mwandesha mashtaka Maulid Manu ambaye ni Mkaguzi wa Polisi (INSPEKTA) aliiambia Mahakama hiyo kuwa Bw. Jumanne Hassan alimbaka binti mwenye umri wa
miaka (12) ambaye jina lake limehifadhiwa na ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Liganga iliyopo
wilayani kongwa.
Mwendesha mashtaka huyo wa
Polisi, aliieleza mahakama kwamba Bw.
Jumanne Hassan alitenda kosa hilo kwa kumvizia binti huyo aliyekuwa anatoka
kununua mahitaji ya dukani alipokuwa ametumwa kisha kumkamata mkono na kumvutia katika chumba cha rafiki
yake kilichokuwa jirani na eneo hilo kisha kumbaka
na kumtishia kwamba akipiga kelele atamuua.
Alieleza hayo mbele ya mbele ya hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kongwa Bw. Godfrey Pius, aidha alisema tukio hilo
lilitokea Novemba moja, mwaka jana (2011)
majira ya sa mbili na nusu usiku katika eneo la kijiji cha Liganga, Kata ya
Chitego na Tarafa ya Nzoisa Wilayani Kongwa.
No comments:
Post a Comment