Mwakilishi wa ITV mkoani Mara Bw George Marato akifanya Mahojiano na Mkuu wa Mafunzo wa DASIP Bw Julius Sokono |
Musoma,
JUMLA ya masoko saba ya kisasa ya mazao ya kilimo na mifugo yatakayoghalimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 3.5 yanatarajiwa kujengwa na benki ya Maendeleo Barani Afrika (ADB) katika Wilaya sita zinazopakana nanchi jirani za Kenya na Uganda.
Ujenzi huo unalenga kutatua changamoto kubwa ya ukosefu wa masoko ya mazao inayowakabili
wakulima na wafugaji katika maeneo hayo.
Mkuu wa
mafunzo wa Mradi wa Uwekezaji katika
kilimo Wilayani (DASIP) kanda ya ziwa Julius Sokono aliyasema hayo juzi mjini
hapa katika mkutano ambao umeshirikisha watalaam wa sekta kilimo na mifugo
kutoka halmashauri 28 za mikoa ya Mara,Kagera,Kigoma,Shinyanga na Mwanza.
Alisema
mchakato wa ujenzi wa masoko hayo ambalo kila moja linatarajia kugharimu
milioni 500 umeanza kwa kuhusisha wilaya za Tarime (Mara) Ngara,Karagwe,misenyi(Kagera
na Kahama (Shinyanga) pamoja na Kasulu mkoani Kigoma umeanza huku jamii
ikitakiwa kuchangia asilimia 20 za mradi.
“Tayari
mchakato wa ujenzi wa masoko hayo ya kati huko katika hatua za mwisho kwa
kutangaza zabuni za ujenzi sisi dasip ambao ndio tunasimamia ujenzi huu tunaamini
kuwa kukamilika kwa ujenzi huu kutafungua fursa kwa wafugaji na wakulima kupata
soko la uhakika jambo litalowawezesha kujiongezea kipato na kupunguza umasikini”alisema
Alisema mradi wa dasip ambao ndio unasimamia ujenzi wa masoko
hayo,tayari umetekeleza miradi zaidi ya 2500 na kuunda vikundi 11,375 katika
vijiji 780 vya halmashauri 28 katika
mikoa hiyo mitano,lengo likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya
kilimo na mifugo na kukuza kipato cha wananchi walio ndani ya mradi
“Kupitia (DASIP) wakulima na wafugaji 252,836 wamepatiwa mafunzo mbalimbali yakihusisha vijiji hivi 780 vya katika halmashauri
28 nchini yaliyohusu kanuni za msingi za uzalishaji wa mazao,ufugaji wa kuku na
mbuzi pamoja na kuwezeshwa kuunda vikundi hivyo 11,375 vikiwa katika eneo ya mradi”alisema.
Alisema wakulima
hao pia wameweza kunufaika na mafunzo ujasilimali,matumizi bora ya mbolea na
udhibiti wa wadudu na magonjwa kupitia mashamba darasa wanatoka katika
halmashauri hizo za mikoa ya hiyo ya Mara,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Mwanza.
Sonoko alisema
pamoja na mafunzo hayo Dasip kati ya miradi hiyo zaidi ya 2500 ambayo
imetekelezwa na Dasip katika vijiji hivyo 205 ni majosho ya kuogeshea mifugo,masoko
150,malambo ya maji 160,maghala ya vyakula 162 na miradi ya midogo ya
umwagiliaji 34.
Aliongeza
kuwa kupitia vikundi hivyo wakulima wameweza kupanunuliwa mashine za kusaga
440,trekta ndogo za kulimia power tillers 350 pamoja na mashine 36 za kuchakata
mihogo ambayo imesaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na
mifugo sambamba na kuongeza kipato kwa wananchi.
Awali
akifungua
mkutano huo kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Mara,Mhandisi wa Maji
Mkoa Eng Mathayo Athuman,aliwataka wataalam hao kutumia mkutano huo
kuweka
mipango ya kuwezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili sektsa
ya
kilimo na ufugaji ili kuleta mabadiliko yenye tija kwa wakulima na
wafugaji
katika maeneo yao.
Alisisitiza
wataalam hao kutumia mafunzo hayo pia kukabiliana na changamoto ambazo
zimesabisha miradi mingi ambayo imejengwa kupitia chini ya Dasip kuwa chini ya
kiwango huku mingine kushindwa kutumika hadi sasa.
“Ni lazima
tujue kuwa serikali yetu haiwezi kuendelea kukopa fedha na sisi kama viongozi
wa umma tukaziacha zikapotea na wananchi wakaendelea kuteseka na baadaye
wakalipa mikopo ambayo haikuwanufaisha”alisisitiza katibu tawala mkoa wa Mara
katika hotuba yake hiyo.
No comments:
Post a Comment