WANAFUNZI WA TARIME HIGH SCHOOL |
WAUMINI WA KANISA LA ANGLICAN NAO HAWAKUWA NYUMA |
POLISI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME |
WATOTO WANAFUNZI WA SHULE NAO WALISHIRIKI |
KAIMU KAMANDA ZACHARIA AKIFAFANUA JAMBO |
ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA TARIME DK.MWITA AKILI AKISOMA HOTUBA KATIKA UFUNGUZI WA OFISI YA DAWATI LA JINSIA NA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA |
Na Shomari
Binda,Tarime
Askari polisi
wanaohudumia kitengo cha dawati la Jinsia Wanawake na Watoto wametakiwa kuwa na
kauli nzuri wanapokuwa wanawahudumia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya ukatili
wanapowafikia.
Kauli hiyo
ilitolewa na Askofu wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya
Tarime Dk.Mwita Akili
alipokuwa akifunga siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijnsia sambamba na ufunguzi
wa Ofisi ya dawati la Jinsia katika kituo kikuu cha Polisi Wilayani Tarime
Alisema
wahanga wa Ukatili hawana budi kuzungumza nao kwa unyenyekevu ili waweze kuelezea
kwa umakini yale yaliyowasibu na si vyema kuzungumza nao kwa kuwafokea na
kuendelea kuonekana wanyonge.
Askofu Mwita
alisema kuanzishwa kwa dawati la Jinsia na ufunguzi wa Ofisi hiyo kuwe ni chachu ya kuwasaidia
Wanawake hasa wale wanaokutana na vitendo vya ukatili pale wanapowafikia kutaka
msaada kutoka kwao.
“Watakaowafikia
katika ofisi hii ni sawa na mama zenu,dada ama ndugu kwenu hivyo wasaidieni kwa
kuzingatia maadili ya kazi na kuwa na moyo wa huruma ili wapate faraja na
msifanye kinyume na hivyo.
“Mtu anaye
kutana na suala la ukatili anahitaji msaada na kuwa naye kwa ukaribu naamini
askari Polisi watakao kuwa katika dawati hili tayari wanayo mafunzo namna ya
kuwahudumia wahanga wa Ukatili nawaombea kwa Mungu awape wepesi
katikakutekeleza majukumu yenu ya kazi”,alesema askofu Mwita.
Askofu Mwita
alitumia nafasi hiyo kuihasa jamii kuachana na masula ya Ukatili hasa kwa
Wanawake kwani wanapofanyiwa vitendo vya ukatili shughuli mbalimbali za
kiuchumi zinakuwa hazifanyiki na hivyo jamii kuendelea kuwa masikini.
Alisema upo
ukatili ambao hauzungumziwi sana katika jamii katika suala zima la kumnyima
elimu Mwanamke na kudai kuwa hakuna ukatili mbaya kama huo kwani unakwamisha
maendeleo.
“Mwanamke
lazima apewe elimu pamoja na kumpa nafasi ya kumiliki mali ili aweze kufanya
mambo ya faida katika jamii n asiwe Mwanamke wa kuomba kila kitu kwa Mwanaume
ikiwa hata kama anataka kununua mafuta ya kupikia ama mboga,”alisema
Kwa upande
wake Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Tarime Rorya Sebastian Zacharia
alisema kutokana na askari wanaoshughulika na dawati kupata mafunzo ya namna ya
kufanya majukumu yao anaamini watafanya kwa uadilifu mkubwa.
Alisema
Jeshi la Polisi limeingia moja kwa moja katika mapambano ya ukatili wa Kijinsia
na kudai kuwa jamii inapaswa kushirikiana na Jeshi hilo ili kuweza kutokomeza
matukio ya ukatili katika jamii.
No comments:
Post a Comment