Na Thehabari.com,
Korogwe
BAADHI ya
Wanafunzi waliofanya mitihani wa mchujo wa kidato cha pili kuingia kidato cha
tatu Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe huenda wakazuiliwa kupewa matokeo yao
kutokana na kutokuwa na fomu namba 9 (TSM9) za uzajili katika shule zao.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa
habari hizi hivi karibuni wilayani Korogwe, na kuthibitishwa na Kaimu Ofisa
Elimu Sekondari wilaya hiyo, miongoni mwa wanafunzi ambao wataathirika na tatizo
hilo ni kutoka katika shule za sekondari Bungu, Patema pamoja na Mfundia.
Taarifa
zinaeleza wanafunzi hao waliofanya mitihani yao ya mchujo ya kidato cha bila mapema
kuanzia Novemba 5, 2012 bila ya kuwa na TSM9 namba, hivyo walimu wakuu wa shule
husika kuamriwa wawasilishe namba za wanafunzi hao katika kituo cha kusaishia
mitihani hiyo.
Akizungumzia
tatizo hilo, Kaimu Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Shaban
Shemzighwa alikiri kuwepo kwa tatozo hilo na kudai walipokea malalamiko toka ya
baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili juu ya utata wa suala la TSM9.
Hata
hivyo alisema wanafunzi waliokuwa na utata juu ya suala la TSM9 waliruhusiwa
kufanya mitihani yao ya mchujo na baadaye walimu wakuu wa shule zao kuelekezwa wanatakiwa kuwasilisha
namba za wanafunzi hao kwenye vituo vya kusahihishia mitihani ili waweze
kutambulika.
“Taarifa
za malalamiko zilitufikia na baadhi ya Shule za Sekondari ambazo wanafunzi
walikuwa na matatizo hayo ni Bungu, Patema, Mfundia na nyinginezo, hapa nipo
nje ya kituo cha kazi hivyo ni vigumu kutaja idadi na shule zote,” alisema
Shemzighwa akizungumzia suala hilo.
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na baadhi
ya wakuu wa shule ambao shule zao limetajwa kuwa na tatizo hilo walikwepa
kuzungumzia, huku wakidai hawakuwa na tatizo hilo kwa wanafunzi wao.
Mkuu wa
shule ya Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweli akizungumza na mwandishi wa habari
hizi alipinga shule yake kuwa na tatizo hilo licha ya Kaimu Ofisa Elimu
Sekondari kuitaja shule hiyo pia kukumbwa na tatizo la TSM9 kwa wanafunzi wake
kwenye mitihani ya kidato cha pili iliyofanyika Novemba, 2012.
Jumla ya
wanafunzi wa kidato cha pili 442,925 walifanya mitihani ya mchujo wa kidato
hicho mapema Novemba 5, 2012 na watakaoshindwa kupata wastani wa alama 30
watachujwa na kulazimika kurudia kidato hicho kwa mwaka unaofuata.
No comments:
Post a Comment