Na Mwandishi wa Blog hii
MUSOMA
WANANCHI Mbalimbali mkoani Mara
wameilalamikiaSerikali kwa kutowekeza katika elimu ya juu katika mkoa huu wa
Kihistoria hapa nchini.
Wakiongea kwa Nyakati tofauti na mwandishi wa habari
hii,wananchi hao walisema kuwa msimu huu kwasasa ni msimu wa wanafunzi kumaliza
Shahada zao na shahada za juu lakini kwa Mkoa wa Mara hakuna kitu kama hicho
kinachoonekana hapa.
Walisema kuwa kutokuwepo kwa vyuo vinavyotoa elimu
ya Juu hapa MKoani Mara husababisha hata suala la Maendeleo linakuwa la
kusuasua kutokana na eneo kubwa kutokuwa na Wasomi wa kutosha.
“Kiukweli
hili ni tatizo la Serikali kwani mkoa huu hakuna chuo kinachotoa Elimu ya Juu
hivyo wasomi hakuna na kutokuwepo kwa Wasomi ni tabu maana Jamii itabaki katika
mawazo Mgando” alisema Mzee Magesa John mtumishi mstaafu.
Mzee Magesa alisema kuwa Mikoa mingi Tanzania yenye
vyuo vinavyotoa Elimu ya juu imekuwa na Mwamko mkubwa wa Jamii katika suala la
Maendeleo tofauti na hapa Mara kwani hakuna chuo chochote ambacho kingeweza
kuleta hata changamoto kwa Wazazi kuona umuhimu wa Elimu kwa vijana wao.
Akimuunga kuhusu Suala hilo Mwalimu Emanuel
Ghati naye alisema kuwa ni kweli
kukosekana kwa Chuo kinachotoa shahada katika mkoa huu ni kuendelea kuwatenga
wana Mara katika suala la Elimu,Mwali Ghati alisema kuwa ingekuwa rahisi kwa
watu kujiendeleza wanapotoka Kazini kuliko ilivo hivi sasa ambapo watu wengi
wakipangwa Kikazi Mara hawapendi kufanya kazi mkoa kutokana na kutokuwa na
mambo mengi.
“Hii ni kweli maana kuja kufanya kazi huku
kunapelekea kupoteza fursa nyingi hasa suala la elimu kwani Mkoa kama Mwanza
umeendelea kwa sababu una Vyuo ambavyo kwanza vimesababisha Muingiliano kuwa
mkubwa lakini pia vimesaidia Mwamko katika Jamii” alisema Mwl Ghati.
Naye Juma Jambo akitolea mfano Chuo kikuu cha Dodoma
kilivyojengwa haraka na kuanza kutoa huduma alihoji inakuwa Serikali kupitia
wizara ya Maendeleo ya Jamii,jinsia na watoto inashindwa kupandisha Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Buhare kitoe kiwango cha Digree.
Alisema chuo cha Kikuu cha Arusha kilichopo si
msaada wa wana Mara kwani hicho ni chuo ambacho kipo katika kujenga faida na si
kuwasaidia Watanzania,hivyo Basi Jambo aliongeza kuwa anadhani ni muda muafaka
kwa serikali kuona umuhimu wa kupandisha chuo cha Buhare kutoa kiwango cha
Digree.
“Mbona chuo
cha Dodoma kilijengwa kwa muda mfupi na kuanza kazi iweje sisi Mara
tusahaulike na kwanini Serikali
isikipandishe chuo cha Buhare kutoa digree ? alihoji bwa Juma Jambo mkazi wa
Makoko mjini hapa.
No comments:
Post a Comment