Wednesday, November 21, 2012

MLINZI AUAWA KIKATILI MARA

MUSOMA

Mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya salama iliyoko manispaa ya musoma Mkoani Mara ameuwawa kikatili kwa kuchinjwa shingo akiwa lindo katika Pub inayojulikana kwa jina la Tulivu na watu hao Wanaosadikika kuwa ni Majambazi kuondoka na crate mbili za bia na viti .

Taarifa ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara kamishina  msaidizi  Mwandamizi wa Jeshi hilo Absalom mwakyoma alisema kuwa majira ya asubuhi eneo la barabara ya majita kata ya kamunyonge  manispaa ya Musoma  uligunduliwa mwili wa John Nyanganya ( 22)  mlinzi  wa kampuni ya salama security ukiwa umekatwa shingo .


Taarifa hiyo imeendelea kusema kuw uchunguzi umeonyesha  kwamba  wauaji hao walivunja  pub hiyo ,baada  ya kumuua  na kuiba  crate mbili za bia  na viti vya plastiki saba  venye  thamani ya shilingi laki moja na elfu sabini.

Katika taarifa hiyo ya Kamanda Mwakyoma alisema kuwa  ufuatiliaji  wa kina  unafanyika katika kuwabaini  wahalifu hao waliofanya unyama huo ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kufuatia hali hiyo mpaka sasa  Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani hapa akiwa na nondoo tatu ,mtarimbo pinde na mishale mitatu ,kirungu  na nguo za kike ambapo insemekana kuwa Wahalifu hao walivaa nguo za kike kuficha sura zao.

No comments:

Post a Comment