Monday, October 1, 2012

WATU 63 WAMENUSURIKA KUFA BAADA YA BASI LA ADVENTURE KUTOKA MWANZA KWENDA KIGOMA KUWAKA MOTO.

Baadhi ya wananchi wakipakua badhi ya mizigo ambayo imesalia ndani ya basi hilo.
 
Watu 63 wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mwanza kwenda mkoani Kigoma, kuwaka moto.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne na nusu asubuhi katika kijiji cha Nyantakala wilayani Biharamuro, Mkoani Kagera, likihusisha gari aina ya Scania lenye namba T 928 AVP, mali ya Kampuni ya Adventure ya jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka wilayani Biharamuro, watu 8 kati yao wamejeruhiwa kwa moto na wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe, mkoani Geita, kwa matibabu zaidi.
Chanzo ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika betri ya Gari hilo, na mpaka sasa gharama halisi ya mali za abiria zilizoteketea kwa moto bado haijajulikana.

.
Mwonekano wa basi la adventure kwa mbele baad ya kuungua.

Mizigo iliyokuwa ndani ya buti ikiendelea kuteketea.
Hii ndiyo hali halisi ya ajali ya Adventure

1 comment:

  1. Poor bus, Thanks that there's no fatalities, there's lack of used cars, bus, and other vehicles - only few were injured!

    ReplyDelete