Thursday, October 4, 2012

TAMASHA LA MTIKISIKO 2012 NA RADIO EBONY FM LAZINDULIWA HEWANI RASMI


 Promotions Manager wa EBONY FM Bonny Zacharia Nyatogo (aliyekaa kulia) akijiweka sawa tayari kwa uzinduzi wa Tamasha la Mtikisiko hewani
Mratibu mkuu wa Tamasha  hilo Bw Eddo Bashiri akielezea utamu wa mambo utakavyo kuwa mwaka huu
Timu nzima ya watangazaji wa Radio Ebony Fm wakiwa studio katika uzinduzi wa Mtikisiko 2012

Radio Ebony FM yenye makao yake makuu mkoani Iringa na inayorusha matangazo yake katika  masafa ya 87.8 (Iringa), 88.2 (Makambako), 94.7 (Mbeya), 91.6 (Dodoma), 95.4 (Morogoro) na 102.2 (Songea) Oct 01 kupitia kipindi chake cha mchana "THE SPLASH" imezindua hewani (on air launching) TAMASHA lake kubwa la kila mwaka maarufu kwa jina la "MTIKISIKO" ambalo linatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu na kupita karibu sehemu zote inaposikika redio hiyo.

          Akizungumza katika uzinduzi huo Promotions Manager wa EBONY FM Bonny Zacharia Nyatogo amesema, mwaka huu EBONY FM ikishirikiana na kampuni mama ya burudani EBONY ENTERTAINMENT wamejipanga vya kutosha kukata kiu ya burudani kwa wapenda burudani wote kwenye mikoa ya Nyanda Za Juu Kusini ambayo wana uhakika haijakatwa bado.
         
Mratibu mkuu ni Eddo Bashir kama ilivyo kwa miaka iliyopita, naye amesema maandilizi ya TAMASHA hilo yameshaanza na muda wowote kuanzia sasa ratiba rasmi itatangazwa hasa tarehe na maeneo TAMASHA hilo litakapopita. Kauli mbiu ya TAMASHA hilo mwaka huu ni "Ndo Vileee..!!!"
         
 Tamasha la "MTIKISIKO" kihistoria lilianza mwaka 2007 wakati huo likiitwa "PAMOJA TIME" ambapo mwaka 2008 lilibadilishwa jina na kuanza rasmi kuitwa "MTIKISIKO"...nia na madhumuni ya TAMASHA la "MTIKISIKO" ni kukutana pamoja na wasikilizaji wa ukweli wa EBONY FM na kurudisha kwao LOVE wanayotoa kwa redio.

No comments:

Post a Comment