Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi
la Polisi zanzibar limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa
Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea
siku kuu ya Eddi el Haji kwa usalama na amani.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
amezitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia
Ijumaa wiki hii hadi Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi
Mmoja hadi Viwanja vya michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya
Baraza la Wawakilishi la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara
ya ya kutoka Ukumbi wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.
inspekta
Mhina, amesma kuwa barabar hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00
arasili hadi saa 4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa
wamesharejea majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.
Awali
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mjini Magharibi Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa
sherehe hizo zitaadhimishwa kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza
Ijumaa ya Oktoba 26 hadi Jumatatu ya Oktoba 29 2012.
Katika
hatua nyingine Kamanda Aziiz amesema Jeshi la Polisi mkoani humo
litaweka vituo vidogo vya Polisi katika maeneo yote ya viwanja vikubwa
vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu kwa lengo la kuwahakikishia
wananchi ulinzi wa usalama wao pamoja na mali kwa wakati wote wa
sherehe hiyo.
Kamanda
huyuo amevitaja viwanja vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa kwa ajili
ya sherehe hizo za Eddi El Haji kuwa ni Mnazi Mmoja, uwanja wa
Demoklasia, Jamhuri Garden, Forodhan Park, Kiembe Samaki, Nyarugusu,
Maungani na Bububu Meli nne.
Kamanda Aziz amesema Kiwanja cha michezo cha Kariakoo mjini Zanzibar kwa mara nyingi hakitaweza kutumika kutokana na kuharibika.
Amewataka
waqzazi na walezi kutowapa vijana wao makundi makubwa ya watoto wadogo
ili kuepuka kupoteana katika viwanja hivyo ambavyo mara nyingi vinakuwa
na umati mkubwa wa watu.
Amewakumbusha
wazazi na walezi hao pia kutowaruhusu watoto wao kwenda karika fukwe za
bahari kuogelea pasipo uwangalizi wa watu wazima kwani amesema kuwa
uzoefu unaonyesha kuwa watoto huzama na kufa maji baharini pasipokuwa na
uwangalizi katika nyakati za siku kuu kama hizi.
Hata
hivyo Kamanda Aziz amewataka wazazi kuwaelimisha watoto wao kuwa
wanapobaini kupotezana na ndugu na jamaa zao wafike katika vituo hivyo
vidogo vya Polisi na yeyote atakayepotelewa aweze kufika hapo kwa
utambuzi na kumpata mtoto wake.
Amewakumbusha
wananchi kutoziacha nyumba na sehemu zao za biashara pasipo na
uwangalizi wa kutosha wanapotoka kwenda katika viwanja vya burudani ili
kuepuka kuwapa wezi fursa ya kupora mali zao.
Kwa
upande wa madereva kamanda aziz amewataka madereva wote kuendesha vyombo
vyao kwa mwendo wa kadri na kuepuka kuvunja sheria, taratibu na kanuni
za usalama barabarani na kwamba kwa yeyote atakayekaigi agizo hilo hatua
kazi zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kukamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Visiwani
Zanzibar sherehe za Eddi El Fitri na Iddi El haji ndizo sherehe kuwa
kupita zote za kiserikali na husherehekewa kwa muda wa siku nne
mfululizo katika viwanja mbalimbali ingawa utaratibu huo wa kusherehekea
hauingiliani na na ule uliopo kwenye kalenda ya Serikali.
Mwisho
VITAMBULISHO VYA TAIFA
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Zaiidi
ya aslimia 80 ya wakazi wa wilaya ya Kusini Unguja Zanzibar wamejitokeza
kujiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa wengi wao wakiwa ni vijana.
Mkurugenzi
wa Vitambulivyo vya Taifa Zanzibar Bw. Vuai Mussa Suleiman, amesema
kuwa zoezi hilo lililoanza mwanzoni mwa mwezi huu limeonyesha mafanikio
na Jumatatu ijayo ya Oktoba 29, 2012 zoezi hilo litaingia katika wilaya
ya Kati katika mkoa huo wa Kusini Unguja.
Bw.
Vuai alikuwa akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari aliofuatananao
katika ziara ya pamoja ya kuvitembelea vituo hivyo vya kujiandikishia
katika wilaya ya Kusini unguja zoezi ambalo lilianza Oktoba 15, mwaka
huu na linatarajiwa kumalizika kesho Alhamisi Oktoba 26, 2012.
Bw.
Vuai amewataka wananchi wa wilaya zingine kujiandaa kwa kupiga kopi
baadhi ya vielelezo muhimu vikiwemo vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa
ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo.
Wakati
wa ziara hiyo baadhi ya wasimamizi na masheha waliopo katika vituo hivyo
wameelezea mafanikio na changamoto zinazojitokeza ambapo wamesema
baadhi ya watu wanaofika kujiandikisha hawaelewi hata maana na foto
kopi.
Msimamizi
wa Kituo cha Bwejuu Bw. Khamisi Mabrouk Mbaraka,baadhi ya watu
wanaofika katika vituo vyao wanapeleka hati halisi pasipo na kopi.
Nao
baadhi ya Mashehe wamesema kuwa hakuna uwezekano wa mtu asiyehusika
kujipenyeza na kujiandikisha kwa sababu watu wote wakiwemo wasio na
vitambulisho vya Uzanzibar Mkazi wanaoshi katika shehia zao
wameorodheshwa majina na kwamba ikijitokeza utata Sheha anawajibika
kulitatua kwa kupitia kumbukumbu za wakazi wa eneo lake.
Akizungumza
katika kituo cha Bwejuu, mmoja ya watu waliofika kujiandikisha Bi.
Mwakito Mkadamu, ameelezea umuhimu wa vitambulisho hivyo kwa jinsi
alivyoelimishwa kupitia vyombo vya habari na kusema kuwa kinaweza
kumsaidia katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na kiuchumi.
Miongoni
mwa watui wanaojiandikisha kupata vitambulisho hivyo wapo wa kutoka
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara wanaoishi Zanzibar kwa shughuli
binafsi na za kikazi.
No comments:
Post a Comment